HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 21, 2019

BENKI YA MAENDELEO TIB YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUINGIA MKATABA WA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (katikati) akimkabishi mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Charles Singili (kulia) mara baada ya kuuzindua mkataba huo. Uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya Benki ya Maendeleo ya TIB.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto) akimkabidhi nakala ya mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) Bw.Joseph Kidaha (katikati) mwakilishi wa wateja waliohudhuria uzinduzi rasmi wa Mkataba huo. 
 Mkurugenzi, Mkakati na Mahusiano ya Kibiashara, Bw. Patrick Mongella (kulia) akipokea nakala za Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Charles Singili (katikati) akionesha mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) mara ya kukakidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto). Anayeshuhudia ni mmoja wa wateja wa benki hiyo, Bw.Joseph Kidaha (kulia).
 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya TIB wakifuatilia uzinduzi Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter).
Baadhi ya wateja wa Benki ya Maendeleo ya TIB wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (katikati waliokaa) pamoja na menejimenti ya benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Charles Singili (wapili kulia waliokaa).

Na Mwandishi wetu
Benki ya Maendeleo TIB (TIB Development Bank) imeadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza kuadhimishwa tarehe 16 Juni, 2019 kwa kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customers’ Service Charter) ili kuendeleza kutoa huduma bora na zenye viwango kwa wateja wake.
Akizungumza wakati wa unzinduzi wa Mkataba huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Dkt. Mary Mashingo amesema kuwa malengo ya Mkataba huo ni kuendeleza kutoa huduma bora bila ya upendeleo, kwa heshima na kwa haraka.
“Huu ni Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo TIB unaakisi dhamira ya dhati ya Benki ya kuwahudumia wateja bila ya upendeleo, kwa heshima na kwa haraka. Mkataba huu una ahadi za huduma mahsusi na za hiari.
Aliongeza kuwa Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo TIB unatambua wateja wetu wana haki ya kuelewa kiwango cha huduma kinachotolewa na Benki yao kwa wakati wote.
Kwa mujibu wa Dkt. Mashingoo, Benki iko tayari kupokea maoni ya namna ya kurekebisha na kuboresha zaidi huduma zake.
“Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo TIB, tumejipanga kusimamia kwa dhati utekelezaji wa mkataba huu katika kutekeleza dhamira  ya Mheshimiwa  Rais ya  kuwa  na  taasisi za umma zinazowahudumia  wadau wake. Watumishi  wa  Benki mnatakiwa kufanya kazi  kwa weledi,  juhudi,  maarifa  na uadilifu  mkubwa.  Pamoja na utoaji wa huduma bora, kwa haraka na kwa staha ili kuwaondolea wananchi usumbufu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Charles Singili alisema kuwa TIB imejidhatiti katika kuimarisha mahusiano nawateja wake, hivyo kuzinduliwa kwa Mkataba huu kutachochea utendaji kazi wake ikizingatiwa kuwa benki hiyo muhimili muhimu katika kuunganisha Serikali na Sekta Binafsi.
“Zipo Benki za biashara lakini hii ya TIB ni tofauti kabisa kwa kuwa yenyewe imejikita katika kuleta maendeleo kwa wateja na watanzania kwa ujumla. Hivyo, mkataba huu utaimarisha mahusiano na wateja wetu,” amesema.
Ameongeza kuwa TIB ni benki kiunganishi muhimu kati ya Serikali na Sekta Binafsi, kwa kuchagiza uchangiaji kwa kiasi kikubwa katika masuala ya uwekezaji.
Akizungumzia kaulimbiu ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019, isemayo “Uhusiano kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Kujenga utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utoaji wa Huduma Jumuishi.” Bw. Singili ametoa wito kwa vijana kutumia uwepo wa taasisi wezeshi ili waweze kujikwamua katika kuinua vipato vyao na taifa kwa ujumla.
“TIB tumejikita katika kuwasidia vijana waweze kusimamia misingi ya utawala bora lakini pia kuangalia kwa namna ambavyo wanaweza kuzalisha mazao mbalimbali hali inayoweza kuwasaida kutimia malengo yao binafsi na ya serikali kwa ujumla hasa kupitia mkakati wa Tanzania ya viwanda,’’ alifafanua.
Kwa upande wa wateja wa benki hiyo waliowakilishwa na Bwa. Joseph Kidaha amesema kuwa, mkataba huo una maana kubwa kwa wateja wa benki hiyo huku akisisitiza kuwa,  ukisimamiwa vizuri utaleta manufaa makubwa kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.
“Ni jambo zuri kuona mahusiano mazuri yanatengenezwa kati ya benki na wateja wake, hiyo itaamsha ari kwa watu katika kuitafuta hudumu ya benki hii na tulio wengi kutimiza matarajio tuliyojiwekea ,’’ alisema.
Bwana Kidaha aliwataka wadau kuja kukopa katika benki ya TIB na kufanya marejesho kwa muda unaostahili ili kuwafanya watanzania wengi waendelee kunufaika na mikopo ya benki ya maendeleo (TIB)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad