HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 2, 2019

WAZIRI JAFO KUZINDUWA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU HANDENI, TANGA

Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) linalotarajia kufanyika katika Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga. Kulia ni Mwenyekiti wa GAWE, James Ogondick na Ofisa Utetezi TEN/MET, Bw. David Sizya (kushoto). 
Mwenyekiti wa GAWE, James Ogondick (katikati) akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) linalotarajia kufanyika katika Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga. Kushoto ni Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga. 
Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga (kushoto) akijibu maswali ya wanahabari katika mkutano huo. Kulia ni Mwenyekiti wa GAWE, James Ogondick. 

Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo (TAMISEMI), anatarajiwa kuzinduwa maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) mkoani Tanga yatakayofanyika  Wilayani Handeni.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea shughuli mbalimbali zitakazoambatana na maadhimisho hayo.

Alisema shughuli za maadhimisho za mwaka huu zitaanza Mei 6 hadi 10, 2019 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chanika, huku yakiambatana na mikutano vijiji mbalimbali kwa madhumuni ya kuhamasisha wanajamii kuhusu ushiriki wa pamoja na serikali katika kuboresha elimu iliyojumishi na endelevu.

"...Tarehe 10 Mei itakuwa ni kilele cha wiki ya uhamasishaji wa Elimu. Mgeni na mgeni wa Heshima atakuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Kamati ya Maandalizi ya TEN/MET imeamua Kauli mbiu kwa Tanzania iwe ni: “ELimu Bora, Haki Yangu”.

Mratibu huyo wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Wayoga alisema kwa mwaka jana maadhimisho hayo yalifanyika mkoani Singida Wilaya ya Mkalama ambapo yalileta mabadiliko makubwa chanya.

Alibainisha kuwa Mkoa wa Tanga na hasa Wilaya ya Handeni imechaguliwa kuwa sehemu ya kufanyia maadhimisho na kamati ya maandalizi kutokana na juhudi zinazofanywa na wilaya hasa katika upande wa elimu jumuishi.

Aidha akifafanua zaidi, Mwenyekiti wa GAWE, James Ogondick aliongeza kuwa maadhimisho ya Juma la elimu (GAWE) ni tukio la alama kwa mashirika yasiyokuwa ya kiselikali (CSOs) yanayojushughulisha na elimu.

Aliongeza kuwa katika maadhimisho ya mwaka huu kutakuwa na shughuli mbalimbali yakiwemo maandamano ya wanafunzi, maonyesho ya kazi za asasi za kiraia na za Wilaya ya Handeni, ziara kwa baadhi ya jamii kwa ajili ya midahalo na makongamano ya kuboresha elimu.

" TEN/MET kama AZAKI ina wajibu wa kuunga mkono juhudi za serikali za utoaji wa huduma za jamii hususani elimu bora. Ni matumaini yetu kuwa hizi nguvu za pamoja zitawezesha kuboresha elimu na kufikia malengo endelevu hususani lengo la nne linalohusu utoaji wa elimu bora, jumuishi na endelevu."

Maadhimisho ya Juma la elimu (GAWE) ni tukio la alama kwa mashirika yasiyokuwa ya kiselikali (CSOs) yanayojushughulisha na elimu. Maadhimisho haya yalianza mara baada ya Mkutano Mkuu wa pili wa kiulimwengu ambao ulifanyika Dakar Senegal mwaka 2000.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad