HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 31, 2019

WADAU WA AFYA ZANZIBAR WAKUTANA KUTATHMINI ATHARI NA MATOKEO YA KIAFYA

Na Fatma Kassim
WIZARA ya Afya imesema suala la kukabiliana na Majanga si la Wizara ya Afya pekeake linahitaji mashirikiano na taasisi mbalimbali kwa lengo la kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea.

Akifungua mkutano wa wadau wa afya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum amesema ushirikiano wa taasisi tofauti katika nchi ndio njia pekee itakayowezesha kuondosha hali ya hatari.

Alifahamisha kwa sasa Zanzibar imejiweka tayari katika kukabilina na hali ya majanga mbalimbali ikiwemo ya maradhi ya miripuko ambapo katika maradhi ya kipindupindu wameweza kupigahatua kubwa ya kuyaangamiza kutoka na ushirikiano uliopo baina ya taasisi mbalimbali ikiwemo Halmashauri na Wilaya.

Amesema Wizara ya afya itahakikisha inashirikiana na wadau wote ikiwemo washirika wa maendeleo wakiwemo Shirika la Afya Duniani WHO katika kujiweka tayari na hali ya majanga ya maradhi ya miripiko yatakapo tokea ili yasiweze kuleta athari nchini.

Amezitaka Tasisi zote husika kupanga mipango madhubuti itakayo saidia kukabiliana na hali yoyote ya hatari, majanga sambamba na kuondosha kabisa maradhi na kuepuka miripuko.

Nae Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani aliyopo Zanzibar Dk. Andemichael Ghirmay amesema kutokana na majanga yanayongezeka Duniani kote ni vyema kuwepo kituo cha kuratib matukio ya kiafya Wizara ya Afya alishauri.

Ameiomba Wizara ya afya kwa kushirikiana na sekta mbalimbali Kuchukua hatua za makusudi za kuanzisha vituo vya dharura sehemu tofauti ambavyo vitatumika katika kukabiliana na majanga mbalimbali pindipo yatatokea.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid akifungua warsha ya wadau wa kutathmini athari za matukio ya Kiafya uliofanyika katika ukumbi wa Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Watoto Kidongochekundu Mjini Zanzibar.
 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Ofisi ndogo ya Zanzibar Dr. Andemichael Ghirmay akisoma hutuba yake katika Mkutano wa wadau wa afya na kutoa pendekezo la kuwepo kituo cha kuratib matukio ya kiafya Wizara ya Afya.
 Dkt. Mlenge Mgendi akiwasilisha rasimu ya mwazo ya ripoti ya wadau wa Afya ya kutathmini athari na matukio ya kiafya Zanzibar.
 Baadhi ya wadau wa Mkutano wa kutathmini athari na matukio ya kiafya Zanzibar wakifuatulia mkutano huo.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid (watano kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na wadau wa afya kutoka taasisi mbalimbali. Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad