HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 20, 2019

TIRA yazindua kanuni za bima kupitia benki

Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zimezindua Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations).

Akizindua rasmi kanuni hizo Jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Yamungu Kayandabila amezitaka taasisi za fedha na benki nchini kuzizingatia katika utoaji wa huduma zao ili kuongeza ufanisi wa shughuli zao.

Alisema kanuni hizo zitasaidia kusambaza huduma ya bima nchini kwani watu wengi bado hawajafikiwa.

“Ujio wa Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki nchini Tanzania umechelewa kidogo hivyo wadau wana kila sababu ya kuzingatia kwa manufaa ya pande zote watoa huduma na wanufaika,” alisema

Alisema endapo wadau watazizingatia kanuni hizo mapato katika sekta hiyo kiujumla yataongezeka kwa taifa, watoa huduma na watu wengi zaidi watafikiwa na huduma za bima. 
Aidha kwa upande wake 

akizungumza katika hafla hiyo alisema licha ya manufaa lukuki ya uzinduzi wa kanuni hizo pia unalenga kueneleza ajenda ya TIRA ya kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za bima nchini yaani bima kwa wote.

"Tunahitaji kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za Bima (access) nchini kwa kuongeza aina mbalimbali za bima kwa mahitaji mbalimbali, mfano mbadala wa uuzaji na usambazaji wa huduma za bima ikiwemo kutumia benki,” alisema

Kamishna huyo aliongeza kuwa inahitajika teknolojia rahisi na rafiki kwa ajili ya kusambaza bima, kununua bima, kuuza bima, kulipa mafao/madai ya bima, kusikiliza maoni na mahitaji ya wananchi, kuchakata na kuandikisha maombi ya bima," alisema Dk. Saqware.

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa kanuni hizo ni muhimu katika kuendeleza sekta ya kifedha nchini na kusisitiza kuwa pato la taifa, hasa ukizingatia faida nyingi ambazo zitapatikana kwa benki zenyewe na watumiaji wa huduma za bima.

 Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali serekalini, makampuni ya bima, taasisi za kifedha, mawakala mbalimbali na wadau wa sekta ya bima na kudhaminiwa na BoT, Reliance Insurance, Heritage Insurance, Zanzibar Insurance, Chama Cha Watoa Huduma za Bima (ATI), NMB, CRDB Insurance, Metropolitan Life Tanzania, Jubilee Insurance, FSDT, Stanbic Bank, Smart Policy, Alliance Insurance, TPB Bank na Shirika la Bima la Taifa (NIC).

 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dr Yamungu Kayandabila akizidua rasmi Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations) Jijini Dar es Salaam huku wageni wengine wakishuhudia.Uzinduzi huo uliandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). 
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dr Yamungu Kayandabila akizungumza wakati wa uziduzi wa rasmi Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa TIRA, Dk. Baghayo Saqware akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations) uliofanyika jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wadau waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad