HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 18, 2019

TASWIRA MBALIMBALI ZA MKUTANO MKUU WA WANAHISA WA BENKI YA CRDB JIJINI ARUSHA LEO

Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa 24 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, Jaji Mstaafu Augustino Ramadhan akizungumza wakati akiongoza wajumbe wa Mkutano huo kuchangia maoni mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa wakati wa kupitia taarifa ya Mkutano Mkuu, ulifanyika leo Mei 18, 2019 kwenye Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati akitoa taarifa yake kwa mwaka 2018 katika Mkutano Mkuu wa 24 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.

Katibu wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi wa Maswala ya Kampuni, John Rugambo akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 24 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo akizungumza wakati akitoa taarifa ya Fedha katika Mkutano Mkuu wa 24 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza wakati akitoa shukrani na kuwaaga Wanahisa wa Benki ya CRDB katika Mkutano Mkuu wa 24 wa Wanahisa, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa 24 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, Jaji Mstaafu Augustino Ramadhan akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei kwa hotuba nzuri aliyoitoa wakati akiwaaga rasmi Wanahisa wa Benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akimpongeza mbele ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, Mfanyakazi wa Benki hiyo tawi la Bunge Dodoma, Grace Adam kwa huduma bora anazotoa kwa wateja wa tawi hilo na kupandisha cheo kuwa Meneja. Grace amekuwa ni mfano bora katika kuhudumia wateja. 


Sehemu ya Wanahisa wa Benki ya CRDB wakichangia mada mbalimbali zinazoendelea kutolewa katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini ArushaNo comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad