HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 14, 2019

Serikali kutoa elimu ya kwa Wadau wa Sanaa

Na Anitha Jonas – WHUSM
Serikali ya ahidi kuendelea kutoa elimu kwa wadau wa Sanaa nchini iliwaweze kutambua haki na thamani ya kazi zao kufuatia changamoto ya wadau  hao kuuza kazi zao pamoja na umiliki.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Juliana Shonza alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia (CCM) lililohoji serikali inamkakati gani wa kuwasaidia vijana wanaofanya kazi za sanaa na haki zao.

“Serikali kupitia Bodi ya Filamu Tanzania na Baraza la Sanaa la Taifa imetoa elimu kwa wadau 5200 kuhusu masuala ya hakimiliki,hakishiriki,mikataba na makubaliano kupitia mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kuwa walinzi wa kwanza wa kazi na haki zao kwa kuingia mikataba yenye maslai,”alisema Shonza.

Akiendelea kuzungumza  wakati huo wa maswali na majibu bungeni Naibu Waziri huyo alitoa wito kwa wadau wote wa Sanaa kuhakikisha wanasajili kazi zao COSOTA ilikuzilinda na kuweka mazingira mazuri yatakayovirahisishia vyombo vya serikali kusimamia haki zao.

Pamoja na hayo kulikuwepo na swali la nyongeza kutoka wa Mbunge wa Mikumi Joseph Haule (CHADEMA) lililohoji kuwa serikali inampango gani wa kuifanyia marekebisho sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999 inayosimamiwa na COSOTA kufuatia sharia hiyo kuonekana kuwa inamapungufu.

Kufuata swali hilo la nyongeza  Naibu Waziri huyo alifafanua kuwa kwasasa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ipo katika mchakato wa kuihamishia COSOTA katika wizara hiyo kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kwani kumekuwepo na changamoto nyingi kutokana na taasisi hiyo kuwa nje ya wizara na mchakato huo utakapo kamilika serikali itajipanga kufanya marekebisho ya sharia ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Hata hivyo serikali iliendelea kutoa wito kwa wasanii wa kazi za filamu kuandaa kazi zenye ubora na kutumia njia ya mtandao kusambaza kazi zao kufuatia ukuaji wa teknolojia ili kuepuka changamoto iliyopo kwasasa ya kutembeza CD mkononi . 
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza akijibu swali bungeni Jijini Dodoma leo Mei,14 2019 lililohoji Serikali ina mkakati gani wa kuwasadia vijana kupata haki stahiki katika kazi zao za Sanaa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad