HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 29, 2019

RC MAKONDA KUANZA MSAKO WA KUWAKAMATA WAFANYABIASHARA WASIOKUWA NA VITAMBULISHO

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda amesema kuanzia Jumatatu ya June 03 mwaka huu ni marufuku kwa mfanyabiashara wadogo (machinga) ndani ya mkoa huo kufanya biashara bila vitambulisho maalumu vya utambuzi vilivyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli.

RC Makonda amesema kwa kuanzia June 3 utaanza msako wa kuwakamata wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho ndani ya mkoa huo na  kwakuwa walipatiwa muda wa kutosha wa kujisajili na kupatiwa vitambulisho hivyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya  Makonda kubaini uwepo wa wafanyabiashara wanaoendesha shughuli za umachinga bila kuwa na vitambulisho na hiyo ni baada ya kufanya ziara katika mitaa 9 na kubaini kuwepo kwa wafanyabiashara wengi wanaofanya shughuli zao bila vitambulisho vya utambuzi jambo ambalo sio matarajio ya serikali.

Kutokana na hilo  amewataka wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho kufika ofisi za wakuu wa wilaya kuanzia leo Mei 29 ili waweze kusajiliwa na kupatiwa vitambulisho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad