HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 21, 2019

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA KILIMO MALIASILI MIFUGO NA UVUVI IKULU NDOGO KIBWENI ZANZIBAR

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzui Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akiongoza Kikao cha Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar kwa mwezi Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar 21-5-2019, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri.(Picha na Ikulu)
  MAOFISA wa Idara za Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Kilimo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo 21-5-2019.
 WAZIRI wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji Mpango Kazi ya Wizara yake wakati wa mkutano huo uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.
 BAADHI ya Maofisa wa Idara za Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar, wakifuatilia mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo.
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Bi. Maryam Juma Abdalla Mabodi, akiwasilisha Taarifa ya Matumizi na Mapato ya Wizara yake wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Matreka Zana za Kilimo Zanzibar Ndg. Afani Othman Maalim, akichangia wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar. (Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad