Kwa kipindi cha Miezi tisa Julai 2018 hadi Machi 2019 Jumla ya
Mashauri ya ndoa 16832 yalipokelewa ikilinganishwa na mashauri 13382
ya mwaka 2017/18 hali ambayo ni sawa na ongezeko la 34% ya migogoro ya
ndoa hapa Nchini.
Akiongea kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo
ya Jamii Dkt. John Jingu Mkurugenzi wa Watoto wa Wizara hiyo Mwajuma Magwiza aliitaja changamoto ya maadili ya mmomonyoko wa
maadili kuwa chanzo cha migogoro ya ndoa hapa Nchini.
Magwiza aliongeza kuwa Vitendo vya ukatili kwa watoto ndani ya
familia vimekithiri huku wahausika wakubwa wa vitendo hivyo wakiwa
wanafamilia hili likijionesha katika takwimu za Jeshi la polisi za
mwaka 2017 zinaonesha kuwa Jumla ya matukio ya ukatili kwa watoto
13457 yameripotiwa na Jeshi la polisi.
Alivitaja vitendo hivyo kuhusisha ukatili wa kingono wenye matukio
3,583, mimba za utotoni 1,323 akiongeza kuwa taarifa jeshi hilo
imeonesha matukio ya mikoa ya kipolisi yenye ukatili mkubwa kuwa ni
kinondoni matukio 2,426, Dodoma 1,283, Tanga 164, Tameke 984 na Arusha
Matukio 972.
Wakati huo huo Serikali imewataka baadhi ya Wazazi Nchini kuacha
tabia ya kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto wa kike kama ilivyo kwa
watoto wa kiume jambo ambalo linakwamisha juhudi za Serikali katika
kuhakikisha usawa wa kijinsia unatekelezwa katika nyanja zote bila
ubaguzi wa kijinsia.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhandisi Happiness
Mgalula ambaye pia ni Katibu Tawala Masaidizi Mkoa wa Dodoma aliongeza
kuwa ni lazima elimu itolewe kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Aidha Mgalula amewataka wazazi na walezi kutoa kipaumbele cha
elimu kwa watoto wote bila kujali jinsia ikiwa ni hatua muhimu ya
kutekeleza ahadi ya Rais kwa vitendo ya utoaji elimu bure kwa
wanafunzi hapa Nchini.
Mgalula aliongeza kuwa Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la mila
potofu akizitaja mila hizo kuwa ni kuwa ni mimba na ndoa za utotoni,
haki ya wanawake kumiliki ardhi, vipigo kwa wanawake akiutaja mkoa wa
Dodoma kuwa wa pili kitaifa katika vitendo vya ukatili hapa Nchini.
Aidha Mugarula amewataka wanafamilia kuhakikisha wanakuwa ana Afya
bora kwa kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho vya Bima ya Afya, Elimu
na akina mama wajawazito kuhakikisha wanaenda hospitali ili kupata
huduma ya Afya kwa mama na mtoto.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma Happy Hiza
amesema Mkoa wa Dodoma umefanikiwa kutoa elimu juu ya Makosa ya Jinai
kwa maafisa Ustawi na Maendeleo ya jamii na katika ngazi ya Jamii ili
kuwezesha elimu ya malezi na makuzi kwa watoto katika jamii.
Wanafunzi
wa kikundi cha Brass Band kutoka Shule ya Msingi St. Home wakiongoza
Maandamano ya Wanafunzi wenzao katika kilele cha Mazimisho ya Siku ya
Familia Duniani yaliyofanyika leo katika Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Watoto wa Wizara ya Afya kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza akitoa hotuba kwa niaba ya Katibu
Mkuu wa Wizara yake wakati kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Familia
Duniani yaliyofanyika leo katika Mkoa wa Dodoma.
Katibu
Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Happiness Mgalula akitoa hotuba kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati wa kilele cha Mazimisho ya Siku
ya Familia Duniani yaliyofanyika leo katika Mkoa wa Dodoma.
Katibu
Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Happiness Mgalula akivalishwa skafu
na Skauti wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya
Nyerere Square katika Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani .
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Happiness Mgalula
akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Maadhimisho ya
Siku ya Familia Duniani.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
No comments:
Post a Comment