Wilaya ya Kaskazini B imetajwa kuwa Wilaya iliyo chini zaidi katika
kutekeleza zoezi la kuwapatia Watoto wao Vitamin A na Dawa za Minyoo
hivyo juhudi zinahitajika zaidi kuondosha tatizo hilo.
Afisa Lishe Kitengo cha Lishe wa Subira Bakari Ame amebainisha hayo
wakati akitoa takwimu za zoezi lililofanyika Mwezi Disemba mwaka jana
kwa Waandishi wa habari na Wadau wengine wa afya katika ukumbi wa
Hospital ya Wagonjwa wa akili Kidongo chekundu.
Amesema hali hiyo inatokana na sababu mbali mbali ikiwemo uelewa mdogo
wa elimu ya afya na ushirikiano hafifu wanaoupata kutoka kwa Wadau
tofauti wa Wilaya hiyo.
Hivyo amesema ipo haja kufanyika kwa mjadala wa pamoja kubaini chanzo
cha tatizo ili kuifanya Wilaya hiyo kufikia viwango sawa na Wilaya
nyingine.
Kwa upande wao washiriki wa Mkutano huo walipedekeza kutengenezwe
Bajeti maalum ya kuongeza elimu ya Afya kwa Wilaya hiyo.
Aidha wamesema ipo haja ya kuishirikisha jamii yote ikiwemo Wazee na
Walimu wa Madrsa badala ya kuwaachia Masheha na Wajumbe wao kusimamia
zoezi la kuhamasisha jamii kutekeleza zoezi hilo.
Afisa Lishe Kitengo cha Lishe Wizara ya Afya Subira Bakari Ame akitoa takwimu za utoaji wa Vitamin A kwa watoto na dawa za minyoo pamoja na mikakati ya kuboresha zoezi la mwezi wa sita katika Mkutano uliofanyika Kitengo Shirikishi cha mama na mtoto Kidongochekundu.
Maalim wa Madrasatul Nuru Imani ya Taveta Bi. Asha Uwesu Abdalla akichangia kitu katika Mkutano wa kutafuta nyia sahihi yakuwahamasisha wakina mama kuwapeleka watoto wao kupewa matone ya vitamin A.
Afisa Lishe Wilaya ya Mjini Fatma Ally Said akitoa elimu
ya matone ya Vitamin A kwa Wandishi wa Habari na walimu wa Madrasa ili
kusaidia kutoa elimu hiyo kwa wanachi.
Picha na Makame Mshenga.
No comments:
Post a Comment