HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 18, 2019

Ujio wa Sevilla Fc ni fursa ya kukuza Michezo na Kuitangaza nchi: Shonza

Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza amesema kuwa ujio wa timu ya Sevilla Fc kutoka Laliga nchini Hispania ni fursa kubwa ya kukuza na kuendeleza michezo hapa nchini.

Naibu Waziri ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati Kampuni ya SportPesa ilipotangaza ujio wa Klabu hiyo kubwa inayoshiriki ligi ya Laliga ikiwa nafasi ya tano ambayo inatarajiwa kuja nchini Mei 21 kucheza na mojawapo ya timu kubwa inayoshiriki ligi Kuu hapa nchini.
“Ujio wa Sevvila Fc ni fursa kubwa sana kwa nchi yetu kwani itasaidia kutangaza na kuinua wachezaji na ligi yetu Ulimwenguni kote,”alisema Shonza.

Naye Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kingwangalla ameeleza kuwa ujio wa timu hiyo utachangia kutangaza utalii wa nchi yetu na ameahidi kuipeleka kutembelea moja ya hifadhi pamoja na kisiwa cha Zanzibar.
Kwa upande wake Mkurugenzi na Mdhibiti wa Kampuni ya SportPesa Bw. Abbas Tarimba amesema Kampuni yake inaendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza michezo ikiwa ni pamoja na kuleta timu kubwa Duniani ambazo zinatangaza soka la hapa nchini.

“Sevilla inakuja kucheza hapa nchini na timu ya Yanga au Simba ambazo zinatengenezewa mfumo maalum wa kupatikana timu mojawapo kati ya hizo mechi itakayochezwa mnamo Mei 2019”, alisema Bw.Tarimba.
Vilevile Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw.Wilfred Kidau ameeleza kuwa maandalizi ya kuipokea timu hiyo yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na kusajili Mechi hiyo ya kimataifa katika Shirikisho la mpira wa miguu Duniani.
 Naibu waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza akizungumza na Waandishi wa Habari Aprili 17, 2019 Jijini Dodoma kuhusu ujio wa Klabu ya Sevilla Fc kutoka Laliga  unaoratibiwa na Kampuni ya SportPesa ambayo itacheza na timu ya Yanga au Simba Mei 23,2019.Kulia ni Mdhibiti na Utawala  wa Kampuni hiyo Bw.Abbas Tarimba.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Hamis Kingwangalla (mwenye suti ya kijivu) pamoja na Viongozi wa Kampuni ya SportPesa baada ya mkutano na waandishi wa Waandishi wa Habari Aprili 17, 2019 Jijini Dodoma kuhusu ujio wa Klabu ya Sevilla Fc kutoka Laliga  unaoratibiwa na Kampuni hiyo ambayo itacheza na timu ya Yanga au Simba Mei 23,2019.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw.Nicholas William.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad