HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 9, 2019

MHANDISI LUHEMEJA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI 41 YA DAWASA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja  ameanza ziara ya wiki moja ya kutembelea miradi 41 ya mamlaka hiyo inayoendeshwa kwa fedha za ndani.

Ziara hiyo itakayokuwa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani itaangalia tathmini ya miezi sita toka kuanza kwa Dawasa mpya.

Akizungumza kabla ya ziara hiyo, Luhemeja amesema kuna miradi 41 inayotekelezwa kwa fedha za ndani ambapo wametenga asilimia 35 ya mapato yao ya kila mwezi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali.

“Katika kipindi cha miezi tumetumia bilioni 15 kwa ajili ha miradi 41 iiliyopo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji na mingine ikiwa ni mipya itakayotatua changamoto ya maji kwenye maeneo yaliyokosa mtandao kwa muda mrefu,”amesema Luhemeja.

Amesema lengo kuu la Dawasa ni kuwekeza kwenye mtandao kwa kutumia fedha za ndani na kila mwezi wamekuwa wanatumia bilion 3  kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Gezaulole, Chalinze Mboga, Kisarawe, Kibamba, Kiwalani Pahse 3 na miradi mingine.

Luhemeja ameeleza kuwa kwa sasa Mkoa wa Dar es Salaam upatikanaji wake wa maji ni asilimia 85 ambapo kwa siku yanazalishwa maji Lita milioni 502 kutoka kwenye mtambo wa Ruvu Juu, Ruvu Chini, Mto Kizinga na Visima vilivyojengwa na jamii au watu binafsi.

Ziara ya Afisa Mtendajj Mkuu itamalizika mwishoni mwa wiki hii na inatarajia kuleta faraja kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ikiwemo Mabwepande, Bunju na Kitunda ambapo mradi wao unatarajiwa kukamilika Ijumaa hii na wananchi watapata maji kuanzia Jumamosi.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)Mhandisi Cyprian Luhemeja akiangalia uchimbaji wa mitaro kwa ajili ya ulazaji wa mabomba ya inchi 8 yeye urefu wa Kilomita 2.5 kutoka kwenye tenki la Mabwepande kwa ajili ya kuanza kuwahudumia wananchi wa maeneo ya Bunju, Kitunda na Mabwepande.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akikagua toleo linalopokea maji kutoka Tanki la maji la Mabwepande litakalohudumia wananchi wa Bunju, Kitunda na Mabwepande.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad