HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 21, 2019

JUVENTUS YAWEKA REKODI MPYA ULAYA NA ITALIA BAADA YAKUTWAA TAJI LA LIGI MARA 8 MFULULIZO


Na Bakari Madjeshi wa Michuzi TV 

Klabu ya Soka ya Juventus ya Italia imeweka rekodi mpya barani Ulaya na nchini Italia baada yakutwaa taji la Ligi Kuu Soka nchini humo maarufu kama Serie A mara nane mfululizo. Hii  inakuwa timu ya kwanza kuweka rekodi hiyo, ambapo hakuna timu katika Ligi tano bora la Ulaya iliyofanya hivyo. 

Juventus maarufu kwa jina la Bianconeri ilikuwa ikihitaji alama moja tu katika mchezo wake waliotandikwa bao 2-1 na SPAL, hivyo ikashindikana kutangaza ubingwa huo, katika mchezo wake dhidi ya Fiorentina, Juventus iliondoka na ushindi wa bao 2-1, hivyo kutangaza ubingwa huo. 

Katika mchezo huo dhidi ya Fiorentina, Juventus walitoka nyuma kwa bao la Nikola Milenkovic dakika ya 6, kabla ya Alex Sandro kusawazisha dakika ya 37 na bao lakujifunga la Beki wa Kati wa Fiorentina, GermĆ n Pezzella dakika ya 53, hivyo kufanya jumla ya bao 2-1.

Ushindi huo umepelekea Juventus kutwaa taji la Serie A mara 8 mfululizo, rekodi ambayo haijawekwa na timu yoyote katika bara la Ulaya. Ikiwa na mchezo 150 katika Uwanja wake wa nyumbani, imeshinda michezo 127, mabao yakufunga 335.

MAX ALLEGRI AWEKA REKODI YA KOCHA WA KWANZA KUTWAA MATAJI MATANO MFULULIZO 

Kocha Mkuu wa Juventus, Max Allegri baada ya timu hiyo kutwaa Ubingwa wake mara nane mfululizo, anakuwa Kocha wa kwanza kutwaa mataji matano ya Ligi (Serie A).

Allegri anatwaa mataji hayo matano baada yakuachiwa mikoba na Kocha Antonio Conte aliyetwaa mataji hayo mara tatu. 

Rekodi hiyo inamuweka Kocha huyo katika nafasi ya pili, nyuma ya Giovanni Trapattoni anayeshikilia mataji Saba ya Serie A.

Juventus watakabidhiwa Kombe lao katika mchezo unaofuata dhidi ya Atalanta, nyumbani.

Kocha Mkuu wa Juventus, Max Allegri

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad