HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 3, 2019

GULAMALI CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI JULAI MWAKA HUU

* Lalenga kuimarisha sekta ya elimu, Shule  zote za Sekondari katika jimbo la Manonga kushiriki 

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
LIGI ya mpira kwa wanafunzi wa shule za sekondari katika jimbo la Manonga zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwezi Julai mwaka huu na hiyo yote ni kwa malengo ya kuimarisha sekta ya elimu jimboni humo.

Mashindano hayo yaliyopewa jina la Gulamali Cup 2019 yamekuja baada ya mbunge wa jimbo hilo Seif Gulamali kuwezeka zaidi katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha mazingira ya ujifunzaji na miundombinu ya sekta hiyo yanakuwa rafiki kwa wanafunzi na walimu.

Imeeleezwa kuwa mashindano hayo yatawaweka pamoja wanafunzi na walimu pamoja na kubadilishana mawazo na kuzidi kuboresha sekta ya elimu.

Aidha shule zitakazoshiriki mashindano hayo ni sekondari zote za jimbo hilo ambazo ni Choma, Ziba, Misana, Ngulumwa, Mwashiku, Ndembezi, Nkinga, Mwisi, Simbo, Ichama, Igoweto, Sungwizi, Ibologelo, Mwakipanga, Umoja, Ulaya na shule ya sekondari ya Mtakatifu Thomas.

Ligi hiyo itahusisha michezo mbalimbali na washindi watakaoibuka kidedea kujipatia zawadi kutoka kwa Mbunge wao.

Ikumbukwe kuwa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana zaidi ya watahiniwa 250 walipata daraja la kwanza hadi la tatu huku ikielezwa  kuwa jitihada za mbunge wa jimbo hilo katika kuweka miundombinu rafiki ya majengo na nyumba za walimu pamoja na kuwalipia ada wanafunzi wanaofaulu kwenda kidato cha tano imekuwa chachu kubwa  kwa wanafunzi na walimu .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad