HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 16, 2019

GOLIKIPA ALIYEVUNJIKA MGUU HOROYA APEWA MKATABA MPYA...


Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii 

Golikipa wa Klabu ya Horoya Athlètic Club ya Guinea, Khadim Ndiaye ameongezwa mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo baada kuvunjika vibaya mguu wake katika mtanange wa Robo Fainali ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco. 

Kipa huyo wa Kimataifa wa Senegal aliyecheza michezo yote ya Michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Russia ameongezwa mkataba huo kutokana na mkataba wake wa awali kumalizika mwaka huu, Horoya imetaka kuwa na Kipa huyo kwa kumpa mkataba leo April 14.

Mmiliki wa timu hiyo, Antonio Souare amehakikisha Ndiaye anakuwa sehemu ya timu hiyo endapo atastaafu kusakata kabumbu na atapata mafunzo ya Ukocha barani Ulaya. 

Kipa huyo alikutwa na mkasa huo baada yakugongana na mwenzake, Boubacar Samassekou kabla hajatolewa nje na machela katika mchezo waliokubali kichapo cha bao 5-0.

Horoya kupitia Mitandao ya Kijamii imethibitisha kuwa Ndiaye anaendelea kupatiwa matibabu katika Hosptitali ya Cheick Zaidi University mjini Rabat nchini Morocco.Imeelezwa kuwa Kipa huyo alikuwa anaipenda timu hiyo ya Horoya kiasi kwamba hata akipewa mkataba na Barcelona angekataa licha 

yakuachwa kwenye Kikosi cha timu ya taifa cha Kocha Aliou Cisse tangu kumalizika kwa Michuano ya Kombe la Dunia 2018.

Ndiaye alianza kucheza Soka katika timu ya Senegal kabla hajaenda kucheza kwa mkopo katika Klabu ya ASC Linguère kabla hajaenda kucheza kwa mkopo nchini Sweden katika Klabu ya Kalmar FF mwaka 2012.

Alirejea nyumbani nakujiunga na timu ya ASC Diaraf yenye Makao Makuu mjini Dakar ambapo alicheza msimu mmoja nakutimkia Horoya AC n November 2013.

Ndiaye amecheza michezo 28 katika Kikosi cha timu ya taifa, amefanikiwa kuiwakilisha nchi hiyo katika Mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2012 na 2017.


CHANZO: BBC



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad