Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kaabi amewaongoza Viongozi wa
Serikali, Ndugu, Jamaa na Marafiki katika Dua maalum ya kuwaombea
Viongozi mbali mbali wa Kitaifa waliotangulia mbele ya haki akiwemo
Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi.
Dua hiyo ilianza kwa kisomo cha Khitma na kuzuru Kaburi lake huko
nyumbani kwa Marehem Migombani nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akitoa nasaha zake Mufti Kaabi amesema Marehem Aboud Jumbe alikuwa ni
Mtu aliyependa mashirikiano katika kuliongoza Taifa kwa umahiri.
Ame
sema Marehem pia alikuwa kiongozi muadilifu, aliyependa Wananchi wa
Zanzibar washiriki kikamilifu katika kutafuta Elimu ndani na nje ya
nchi ili kuendeleza maendeleo ya Zanzibar.
“Katika kupigania haki ya elimu kwa Wananchi Marehem alishajihisha
wananchi kutafuta Nafasi za kusoma nje Skolaship na ndani ili
kuhakikisha jamii inafaidika na fursa hizo” Alisema Shekh Kaabi
Katibu Mkuu wa Mufti sheikh Fadhil Soraga alisema iko haja kubwa ya
kuwaombea dua viongozi kwani wamefanya mengi mazuri na yanaendelezwa
hadi leo ikiwemo kushajihisha Wananchi kuishi kwa amani na utuluivu.
Amesema kuna umuhimu wa Viongozi waliopo madarakani kuyaendeleza kwa
umakini mkubwa yote mazuri yaliyoasisiwa na viongozi hao kwa faida ya
Kizazi cha sasa na baadae.
Awali Shekh Thabit Nooman Jongo kutoka Ofisi ya Mufti alisema lengo la
dua hiyo ni kuwakumbuka viongozi wote walioshika nyadhifa mbali mbali
za uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao kwa sasa
wametangulia mbele ya haki ili Mwenyezi Mungu awasamehe makosa yao.
Alisema dhamira kubwa ya kuwaombea dua ni kuwakumbuka kwa yale
waliyoyafanya katika nchi hii akiwemo Marehemu Rais Mstaafu Alhajj
Aboud Jumbe Mwinyi kwa mambo mengi yaliyoyafanyika katika uongozi
wake.
Miongoni mwa mambo aliyoyafanya wakati wa uhai wake ni pamoja na
kuwaunganisha wananchi wote wa Unguja na Pemba na kuwa kitu kimoja ili
kuendelea kuishi kwa amani na utulivu kama alivyotaka Marehemu Mzee
Karume.
Ibada hiyo ya kuwaombe Dua Viongozi wa Kitaifa itaendelea katika
maeneo tofauti ambapo itaendelea Chukwani kwa kumuombea marehemu Mzee
Thabit Kombo, na kesho itasomwa Dua ya Marehemu Idrissa Abdulwakil
huko Makunduchi.
Kwa upande wa Pemba Viongozi ndugu na Jamaa wa Marehemu watakusanyika
kumuombea Waziri kiongozi mstaafu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano Dkt Omar Ali Juma huko kijijini kwao Wawi.
Dua hiyo itakuwa endelevu kila ikifika kumbu kumbu ya Mashujaa ambayo
kilele chake hufanyika April saba Kisiwandui mjini Zanzibar
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi akiongoza Viongozi wa Serikali ndugu na Jamaa katika Dua maalum ya kuwaombea Mashujaa ambapo imeanza kwa aliekuwa Rais wa Zanzibar awamu ya Pili Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi hadi kufikia kilele chake siku ya 07/04/2019 Kisiwandui Zanzibar.
Baadhi ya waheshimiwa na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Dua maalum ya kuwaombea Mashujaa ambapo imeanza kwa aliekuwa Rais wa Zanzibar awamu ya Pili Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi hadi kufikia kilele chake siku ya Mashujaa 07/04/2019 Kisiwandui Zanzibar.
Baadhi ya waheshimiwa na wananchi mbalimbali
waliohudhuria katika Dua maalum ya kuwaombea Mashujaa ambapo imeanza
kwa aliekuwa Rais wa Zanzibar awamu ya Pili Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi
hadi kufikia kilele chake siku ya Mashujaa 07/04/2019 Kisiwandui
Zanzibar,
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment