HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 6, 2019

CRDB Insurance Broker Ltd yashiriki Kambi ya Afya ya Mwananchi, jijini Dar

Kampuni ya CRDB Insurance Broker Ltd ikiwa ni mdau mkubwa wa Maendeleo ya sekta ya afya nchini kupitia huduma zake za bima ya afya, imeungana pamoja na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kufanikisha Kambi ya utoaji wa huduma za afya bure (Mwananchi Afya Camp) iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.

Ushiriki wa CRDB Insurance Broker Ltd katika Kambi ya Afya ya Mwananchi ni sehemu ya kutoa fursa ya upatikanaji wa bima za afya kwa Watanzania wengi hasa ukizingatia watu wengi wamekuwa wakishindwa kumudu gharama za matibabu.
Akizungumza mapema leo, Meneja Mkuu wa CRDB Insurance Broker Ltd, Arthur Mosha amesema  kuwa afya ya binadamu ni muhimu kuliko vitu vyote na ili taifa liendelee tunahitaji watu wenye afya njema. Tumeshuhudia taifa likipoteza nguvu kazi kutokana na kukosa huduma bora za matibabu.

Ni matamanio yetu kuwa wananchi wote wawe na afya bora ili tuendelee kufanya kazi na kuzalisha kwa ajili ya taifa na hii ndiyo sababu tumeamua kuwa sehemu ya washiriki wa Kambi ya Afya ya Mwananchi ili kuhamasisha wananchi wengi kufahamu umuhimu wa afya.
 Afisa wa CRDB Insurance Broker Ltd, Clinton Minja akiwapatia maelezo ya huduma za bima wananchi waliotembelea Banda lao wakati wa Kambi ya Afya ya Mwananchi, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Afisa wa CRDB Insurance Broker Ltd, Witness Misese akiwapatia maelezo ya huduma za bima wananchi waliotembelea Banda lao wakati wa Kambi ya Afya ya Mwananchi, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad