HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 8, 2019

Airtel, DTBi yatoa mafunzo kwa wajasiriamali wanawake

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) imemaliza kutoa mafunzo ya Tehama kwa wanawake wajasiriamali yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao.

Mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika kwenye maabara ya Tehama iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama Manispaa ya Kinondoni na yamefikia tamati mwishoni mwa wiki chini ya udhamini wa Airtel kwa kushirikiana na DTBi

Akiongea jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo, Meneja maabara ya Airtel Fursa na ambaye pia alikuwa ni mratibu wa mafunzo hayo Michael Thomas alisema kuwa teknolojia inaweza kuwafanya wajasiriamali kupata na kutumia ujuzi wa mtandao na kupata taarifa au habari ambazo zina umuhimu na tija kubwa kwao. ‘Ni furaha sana kuona wajasiriamali wetu na hasa wanawake wamejitokeza kwa wingi kuja kupata mafunzo ya Tehama ambayo yatawasaidia kuendesha biashara zao kwa njia ya kisasa ya mtandao’, alisema Thomas.

‘Mafunzo haya ya Tehama yamewapa ujuzi wajasiriamali jinsi ya kutumia vitabu vya biashara kwa ajili ya kuhifadhi rekodi zao. Vile vile, yamewapa ujuzi wa kutumia kompyuta na hasa kwenye kufanya mahesabu ya mauzo na manunuzi, alisema Thomas huku akiongeza kuwa hii itakuwa ni fursa ya kipekee ya kukuza biashara zao kwa kutumia njia ya mtandao.

”Natoa rai kwa kwa wale wajasiriamali wanaonza au waliopo kwenye biashara kupata mafunzo ya Tehama kwani itasaidia kuwapunguzia kazi zao na vile vile kukuza biashara kwa njia bora ya kisasa ya mtandao, alisema Thomas.

Thomas alisema kuwa wajasiriamali wanawake wako na hamasa kubwa ya kujifunzi kozi mbali mbali zinazotolewa hapa. Tulikuwa na wajasiriamali wanawake 26 hapa na wote wameonyesha nia ya kweli ya kupata mafunzo, aliongeza Thomas.

Thomas aliongeza kuwa mpaka kufikia mwisho wa mafunzo hayo wajasiriamali hao wameweza kujifunza maana na historia ya kompyuta, kutumia applikesheni na programu tofauti za kompyuta, kutumia teknolojia kutangaza biashara na hasa kwenye face book na instragrams, kutumia kompyuta kuweka rekodi ya biashara zao, kutumia kompyuta kufanya hesabu ili kujua faida na hasara na pia kuweza kuzijua baadhi ya mambo ndani ya kompyuta.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema Airtel pamoja na DTBi zimeweza kuvuta wanafunzi wengi kujifunza Tehama tangu kuzinduliwa kwa maabara hiyo. Tumeweza kutoa mafunzo mengi kwa vikundi mbali mbali ikiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, waalimu na kwa sasa wanawake wajasiriamali. Naomba nitoe rai kwa yeyote ambaye anataka kujifunza Tehama kujitokeza kwani tuna waalimu wanzuri na waliobobea, alisema Singano.

Wakati huo huo, DTBi imetangaza mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wakati wa likizo inayokuja na kuwaomba Wazazi na walezi kuwasajili kwa kupitia www.teknohama.or.tz or www.airtelfursa.com au kwa kutembelea maabara ya Airtel Fursa ambayo ipo kwenye shule ya msingi ya Kijitonyama.
 Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Michael Thomas akitoa maelekeo ya mafunzo ya kutumia kompyuta kwa moja ya wajasiriamali wanawake Joyce Mmasi kwenye mafunzo ya Tehama kwa wajasiriamali wanawake yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yaliendesha na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Michael Thomas akitoa maelekeo ya mafunzo ya kutumia kompyuta kwa moja ya wajasiriamali wanawake Elizabeth Joshua kwenye mafunzo ya Tehama kwa wajasiriamali wanawake yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yaliendesha na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Fedha kutoka Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Makange Mramba (kushoto) akimkabidhi cheti moja ya wajasiriamali wanawake Martha Aloyce baada ya kuhitimu mafunzo ya Tehama kwa wajasiriamali wanawake yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yaliendesha na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Fedha kutoka Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Makange Mramba (kushoto) akimkabidhi cheti moja ya wajasiriamali wanawake Devotha Michael baada ya kuhitimu mafunzo ya Tehama kwa wajasiriamali wanawake yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yaliendesha na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Fedha kutoka Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Makange Mramba (kushoto) akimkabidhi cheti Ali Mohammed baada ya kuhitimu mafunzo ya Tehama kwa wajasiriamali yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yaliendesha na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Matukio Airtel Tanzania Dangio Kaniki.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad