WAZIRI MBARAWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA MAJI WA KISARAWE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 8 March 2019

WAZIRI MBARAWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA MAJI WA KISARAWE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa amefurahishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kisarawe unaoendelea Kwa sasa unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai.

Katika ziara yake aliyoifanya leo kwa kutembelea ujenzi wa tanki la Kisarawe na Kibamba, Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa mradi huu kutasaidia katika utaoji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Kisarawe pamoja na viwanda vilivyopo.

Mbarawa amesema kuwa mradi wa Kisarawe unajengwa kwa fedha za ndani za Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA  na unagharimu takribani Bilioni 10 za kitanzania.

Amesema, adhma ya serikali ni kuhakikisha 2020 wananchi wa mijini wanapata maji wka asilimia 95, Wilaya ni asilimia 90 na vijjjni asilimia 85.

“Malengo ya serikali ni kuona wananchi wote wanapata maji ifikapo 2020, na Mamlaka zote zinatakiwa kuhakikisha malengo hayo yanafanyika kwa jitihada kubwa sana,” amesema Mbarawa.

Akizungumzia siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa kila Machi 08, Waziri Mbarawa amesema kuwa mwanamke ndiyo mtu anayeiangalia familia na malengo ya kumtua mama ndoo chumbani yatafikia ifikapo 2020 na hilo linawezekana kama Mamlaka za Maji zitafanikisha miradi yote ya maji inayotekelezwa kwa sasa.

Msimamizi wa mradi wa Kisarawe Mhandisi Kakwezi Ishmael amesema kuwa muda uliopo kwa sasa ni utekelezaji tu kama maagizo ya Waziri alivyoyatoa.

Baada ya kumaliza kutembelea miradi hiyo, Waziri Mbarawa ameutaka uongozi wa DAWASA kusimamia miradi ili iweze kumalizika kwa wakati ili wananchi waliokaa kipindi kirefu bila kuwa na maji safi na salama.

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiwa anakagua maendeleo ya mradi wa maji wa Kisarawe unaoendelea kwa kasi ukiwa unatarajiwa kukamilia mwishoni mwa mwezi Julai. 
 Msimamizi  wa Mradi wa Maji wa Kisarawe kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Kakwezi Ishmael akielezea mradi mzima wa Kisarawe kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na wanahabari baada ya kumaliza kutembelea mradi wa maji wa Kisarawe  na kasi ya ujenzi unaoendelea, kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Kisarawe kutoka DAWASA Mhandisi Kakwezi Ishmael.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad