HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 25, 2019

SERIKALI KUJA NA SERA YA KUWALINDA WABUNIFU

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

SERIKALI imesema iko katika hatua za mwisho kukamilisha sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu ambayo itatotoa mwongozo wa namna ya utekelezaji wa masuala ya ubunifu na kuwatambua wabunifu kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Pia iko tayari kufadhili bunifu mbalimbali zitakazoondoa changamoto za hali ngumu ya maisha nchini na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Viwanda.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, ameyasema hayo leo Machi 25, 2019 wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na wadau wengine iliyofanyika leo katika ukumbi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.

 Amesema, katika awamu hii ya Tano,  serikali imeweka kipaumbele teknolojia  ili kuongeza chachu ya maendeleo na kufikia  uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

Amesema ili kufikia viwango vya ubunifu vinavyohitajika, serikali imeongeza fedha za ubunifu kwa Costech na kufungua dirisha la kushughulikia masuala ya ubunifu kwani, ubunifu ni kichocheo cha kufikia uchumi wa kati kwa kuhakikisha kunakuwa na mazingira wezeshi kwenye sekta za afya, elimu na viwanda.

Amesema, mapema katika maonesho ya ubunifu yaliyofanyika jijini Dodoma,  washindi 3O walipatikana na kazi zao zitaplekwa atamizi kwa ajili ya kuzifanyia kazi na kutumika katika masuala mbalimbali ya kusaidia nchi

Amesema, amewaasa  wadau wawafikie wabunifu wengi zaidi wa kawaida ambao hawatambuliki  ambao hawatambuliki  ili waweze kutumia ubunifu zao zinazoendana na maisha halisi ya wananchi.

"Wabunifu wengi ni wale wanaokumbana na changamoto za kila siku na kujaribu kuangalia namna ya kuzitatua hivyo wakati mwingine mtakapoandaa wiki ya ubunifu muhakikishe kwamba mnaweka katika maeneo ya wazi kwa ajili ya kuwakutanisha wabunifu wengi na wananchi ili waweze kujua kinachofanyika," ameeleza.

Aidha Ole Nasha amewaasa wabunifu kufanya ubunifu zitakazoendana na changamoto za maisha zilizopo nchini na siyo kufanya bunifu za kujifurahisha sababu wanaweza kukosa soko.

Naye, Kiongozi Mkuu wa mfuko (HDIF), David McGinty amesema wadau wa maendeleo nchini, wamekuwa wakichangia Tanzania kupanda viwango vya kimataifa vya ubunifu kwani  mpaka wanafunzi wa vyuo na sekondari wanahamasishwa kutumia teknolojia kwa ajili ya kujifunzia.

McGinty alisema wanaangalia ubunifu katika sekta za maji, afya, elimu na usafi wa mazingira kwa sababu ni miongoni kwa changamoto zinazoikabili jamii ya kitanzania.

Kwa upande wake,  Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane Miller alisema wanaendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza katika Wiki hiyo ili  kuona kazi zinazofanywa pamoja na kuwaunganisha wabunifu kwa lengo la kuleta mabadiliko ya ubunifu nchini.

Miller amesema ni lazima watumie ubunifu kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Tanzania katika sekta hizo ili kufikia malengo ya uchumi wa viwanda na kwamba kwa kushirikiana na HDIF wataendelea kufadhiki bunifu nchibi ili kutekeleza na kuinua masuala ya ubunifu nchini.

Wiki ya Ubunifu inatekelezwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na wadau wengine.
 Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Olle Nasha akizungumza na wabunifu pamoja na wadau wa kazi za bunifu nchini, wakati akizindua wiki ya Ubunifu leo Machi 25, 2019 katika ukumbi wa Costech jijini Dar es Salaam waliokaa kulia kwake ni Katibu mkuu wizara hiyo,   Dk. Leornad Akwilapo, akifuatiwa na Kiongozi Mkuu wa HDIF David McGinty na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Costech Dk. Amos Nungu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Technolojia (COSTECH), Dk Amos Nungu akizingumza na wabunifu na wadau mbalimbali wa kazi za ubunifu wakati wa uzinduzi wa wiki ya ubunifu iliyoanza  leo Machi 25, 2019  ambapo wabunifu zaidi ya 3000 wa mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Iringa na watakutana na  kubadilishana uwezo kwa lengo la kukuza ubunifu nchini. Kulia kwake aliyevaa miwani ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Olle Nasha akifuatiwa na Katibu mkuu wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk. Leornad Akwilapo, Na kushoto kwake no  Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane Miller na kushoto Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane Miller.
 Kiongozi Mkuu wa mfuko wa ubunifu wa maendeleo(HDIF), David McGinty akizungumza mara baada ya ufunguzi wa wiki hiyo ya ubunifu ambayo imezinduliwa leo Machi 25, 2019 jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wabunifu pamoja na wadau mbalimbali wa kazi za bunifu kutoka ndani na nje ya nchi.

Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane Miller akizungumza mafanikio ya Tanzania yatokanayo na bunifu zinazofanywa na watanzania wakati wa uzinduzi wa wiki ya bunifu, leo jijini Dar es Salaam.

 Jopo la wazungumzaji katika wiki ya Ubunifu wakiwa katika meza ya duara wakiendesha mjadala kuhusiana na maonesho ya ubunifu ambapo wamejadili na kueleza mambo ambayo wangependa Serikali iyachukue na kuyafanyia kazi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad