HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 15, 2019

MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA

 NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 
TIMU ya kitaifa ya kufuatilia na kutatua migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi wakiwemo wakulima, imeingilia kati mgogoro uliodumu kwa miaka saba baina ya wakulima na wafugaji wa Kwala,wilayani Kibaha Mkoani Pwani na kufanikiwa kuumaliza .

Mgogoro huo unabaki historia baada ya wafugaji wa bonde la mto Ruvu  ,Mwembe Ngozi kupewa agizo la kuondoka na kuhamia eneo la Waya,  ranchi ya Taifa NARCO iliyopo Ruvu ili kuwaacha huru wakulima ambao walikuwa wakipata hasara kutokana na mazao yao kulishiwa mifugo.  

Mkurugenzi msaidizi wizara ya mifugo na uvuvi, ambae pia ni mwenyekiti wa timu hiyo, Dr. Martin Ruheta, aliwataka wafugaji hao akiwemo Sauti Mbili na Masanja Kidirgo ambao wana ng'ombe zaidi ya 500 waondoke kuanzia march 18 mwaka huu. 
Aliwaomba, wafugaji hao na wengine waondoke huku serikali ikiendelea kutafuta maeneo ya kudumu, kwa wale ambao mifugo haitoenea kwenye ranchi hiyo. 

"Timu hii ilianza kazi mwezi octoba mwaka jana, mkoa wa Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya ambapo kwa mkoa wa Pwani walianzia Mkuranga, Rufiji, Kisarawe na Leo tunamaliza mgogoro huu hapa Kwala "alifafanua Ruheta. 

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alibainisha ,kwasasa hawaombi tena, bali kuanzia jumatatu ijayo waondoke na atakaekaidi akikutwa ng'ombe wake atakuwa halali kwake .

Assumpter aliyaasa, makundi hayo yaheshimiane ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima. 

Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji (CCWT) Esta Moreto alisema ameridhishwa na maagizo hayo ila anaomba wafugaji waondoe mifugo na sio makazi yao kwakuwa wengine wana wanawake wajawazito na watoto. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad