HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 14, 2019

KAIMU MKURUGENZI SHABANI MIRAO ALILIA MICHEZO KWENYE HALMASHAURI YA CHALINZE

Karim Juma Lugoba- Chalinze
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Bw. Shabani Mirao amefungua jukwaa la michezo kwenye halmashauri ambalo limeanzishwa kwa kutumia mapato ya ndani ambayo yanasimamiwa na idara ya elimu msingi na kuweza kutoa nia yake ya kujenga timu moja ambayo itakayofanya kushiriki kwenye ligi mbalimbali.Tamasha limefunguriwa lugoba kwenye uwanja wa msingi tarehe 13/03/2019 majira ya saa 10:00

 Mirao aonesha kilio chake kwa vijana kukosa ajira na kusubiria ajira na wakati tunatambua kwamba dunia nzima inachangamoto ya ajira kwasasa njia rahisi kutumia michezo kuweza kupunguza swala la ajira na kujenga afya mwili  na kuweza kupunguza changamoto za uwarifu kwenye jamii zetu .

Hata hivyo Mirao uamkuta kijana ana elimu nzuri tu ukiangaria nafsi zilizotoka na waliomba ni wengi waliomba kuliko nafsi kwanini sisi vijana tusitumie michezo kwa kupata kipato njie ya kutegemea ajira za serikalia tubadirike kulingana na mazingira yalivyo.

Afisa Elimu Msing Mwl. Zainabu Makwinya amesema kwamba idara ya elimu imejipanga kikamilifu kuanzisha ligi ambayo itakayoweza kutoa vijana na kuwa timu ya halmashauri ya chalinze na pia ni fursa kubwa kwa vijana kuweza kupata ajira.

Makwinya amesema kwamba uwamasishaji wa michezo upande kwa wanawake ni mkubwa na hata iyo ligi ikianza lazima wanawake  watashiriki kulingana na michezo yote itakayoanzishwa na tumeshapata wachezaji ambao wanauwezo mkubwa wakucheza kwa upande wa netball .

Makwinya amesema kwasasa jamii lazima ibadiriki kulingana na fikra tofauti za watu kwamba michezo ni burudani hapana kwasasa michezo ni ajira kubwa sana na hata ukiangaria mapato ya wachezaji ni makubwa , Hivyo wananchi naomba watumie fursa hii ambayo idara tunaianzisha.

Afisa  Utamaduni wa Halmashauri ya Chalinze Bi. Ester Kalale amesema kwamba kwasasa wananchi wasiogope kuwatumia wao maana wao wanafahamu aina mbalimbali za michezo na yupo tayari kupitia timu moja hadi nyingine kufundisha aina za michezo .

Kalale amesema fursa kubwa kwa tamasha hili la michezo ambalo limefunguliwa na kuonesha mwanga wa ajira kwa vijana .Pia michezo ndo njia rahisi sana kutambuana kwa haraka na njia ya kudumia amani ya nchi yetu na kuongeza upendo kwa kila mmoja wetu .naomba wananchi wanitumie mimi kwa michezo na kupandisha vipato vya ajira .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad