HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 27, 2019

Jafo ataka ushirikiano zaidi na WFP

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo amewataka Shirika la Chakula Duniani (WFP) kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ili kuendelea kuboresha masuala ya Lishe katika jamii.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa kikao na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid cha kujadili masuala mabalimbali yanayohusiana na Lishe sambamba na miradi inayofadhiliwa na fedha za Umoja wa Ulaya kupitia Shirika la chakula Dunia.
Waziri Jafo amesema tunawashukuru kwa ushirikiano mnaotupatia katika miradi mbalimbali ya Lishe na hakika mmekua na mchango mkubwa katika kuboresha Lishe Tanzania; Kwa kuwa Lishe ni suala endelevu na mtambuka tunaomba muendelee kutoa msaada zaidi wa kifedha na kitaalamu ili  Lishe izidi kuboreshwa katika  jamii.
‘Hatuwezi kufikia Taifa la Uchumi wa Kati endapo  watu wetu hawatakuwa na lishe bora, ili watu wafanya kazi kwa bidii, waweze kuzalisha na kulipa kodi inavyotakiwa ni lazima wawe na Afya bora wakati wote hivyo kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha lishe bora ni vitu muhimu sanakatika kufikia lengo la Kitaifa” alisema Jafo. 
Katika kikao hicho Jafo alizungumzia suala la kuanzisha Siku ya Lishe kitaifa itakayozimishwa kila mwaka ili kuendelea kutoa Elimu kwa Umma kuhusu umuhimu wa Lishe katika maisha ya kila siku ya mtanzania.
Alimtaka Binti Mfalme wa Jorda Sarah Zeid kuendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha siku hii muhimu ya kitaifa itakayoanza kuazimishwa mwaka huu wa 2019.
Naye Binti Mfalme Sarah Zeid amesema amefurahishwa sana na utekelezaji wa miradi ya Lishe inayotekelezwa katika Halmashauri nne Nchini na ameridhishwa na matokeo aliyoayaona kuptia miradi ya wananchi.
Ameahidi kupitia Shirika la Chakula Duniani (WFP) kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mingine itakayoendelea kutekelezwa ila kuhakikisha Lishe inaboreshwa katika Jamii.
Naye Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford ameshema watashiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku la Lishe Kitaifa na watatoa ushirikiano unaohitajika katika kufanikisha siku hiyo.
Shirika la Chakula Duniani (WFP) linaratibu mradi wa Boresha Lishe unaotekelezwa katika Halmashauri nne Nchini ambazo ni Bahi, Ikungi, Singida Dc pamoja na Chamwino.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (kushoto) akisalimiana na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid wakati wa ziara yake Nchini kukagua miradi ya Lishe inayotekelewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP).
 Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid akizungumza na Waziri wa Nchi OR- TAMISEMI Selemani Jafo (Mb) wakati wa ziara yake Nchini kukagua miradi ya Lishe inayotekelewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP).
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford akizungumza wakati wa kikao.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akiwa na  Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid (kushoto) pamoja  na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford .
Katika Picha ya Pamoja ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akiwa na  Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford pamoja na watalaamu wa OR-TAMISEMI pamoja na WFP.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad