HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 6, 2019

FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY YAZINDUA NEMBO MPYA

Baada ya uzinduzi huu ndio muonekano wa Nembo mpya ya Foundation for Civil Society (FCS).

BAADA  ya zaidi ya muongo mmoja na nusu kufikia Azaki nchi nzima,  Foundation for Civil Society (FCS) inajikita katika kuongeza ufanisi na juhudi za kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wote katika kuleta maendeleo nchini.
Hayo yameelezwa mapema leo  jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS  Francis Kiwanga wakati wa uzinduzi nembo mpya ya shirika hilo ambayo itaendana na mabadiliko na mfumo wake wa utendaji.

Amesema kuwa nembo hiyo  itahusisha kushirikiana na taasisi zote za Serikali, Bunge, Sekta binafsi, Asasi za kiraia (AZAKI) ili kufikia Maendeleo endelevu ya dunia pamoja na mpango wa Maendeleo wa Taifa wa kuboresha maisha ya watanzania ifikapo 2025.

Aidha amesema  kuwa kwa sasa FCS itatoa ruzuku kwa wastani wa Asasi 150 kwa pande zote mbili za muungano yaani Tanzania Bara na Visiwani kila mwaka, ambapo hapo awali ilikuwa ikitoa kwa Azaki zaidi ya 5500 zilizokuwa zikihudumia wananchi wa mikoa yote hapa nchini.

Ameeleza kuwa kuwa kiasi cha ruzuku kitaongezeka na kwa sasa taasisi hiyo itatoa ruzuku zenye thamani ya billion 11  kwa mwaka na muda wa mkataba pia utakuwa mrefu hadi kufikia miaka miwili ili kupata matokeo mazuri kwa miradi itakayofadhiliwa na FCS.

Akieleza sababu ya kufanya hivyo amesema kuwa wamejikita katika eneo la utawala bora na maendeleo hivyo siyo rahisi kuboresha maeneo hayo kwa mkataba wa mwaka mmoja au miezi sita tu, Hivyo wameona kuna haja ya kuongeza mkataba na kiwango cha ruzuku katika kufanikisha hilo.

Na mwisho alisisitiza watu kupenda kufahamu  kuwa FCS ipo kwa ajili ya watanzania hivyo waondoe mila potofu ya kuwa ni chombo ambacho hakina ubia na serikali na kwa sasa watafanya mambo mengi mazuri kwa kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society  Francis kiwanga akifafanua kuhusiana na nembo mpya iliyozinduliwa na kusema kuwa wamejizatiti kuwafikia wananchi wengi zaidi katika kuleta maendeleo, leo jijini Dar es Salaam.
Zoezi la uzinduzi wa nembo mpya ya Foundation for Civil Society likifanyika, ambapo taasisi ya FCS imehaidi kushirikiana na serikali katika kuhakikisha ufadhili wao kwa Asasi za kiraia unazaa matunda, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka AZAKI mbalimbali hapa nchini wakifuatilia matukio yanayoendelea katika Tafrija hiyo ya Uzinduzi wa nembo mpya ya FCS.
Baada ya Uzinduzi wa nembo mpya ya FCS kulifuatiwa na tukio lingine la uzinduzi wa tovuti mpya (Website) mpya ya shirika hilo kama inavyoonekana pichani.
Washiriki wa semina wakiendelea kusherehekea tafrija.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa shirika la Foundation For Civil Society. 
Wafanyakazi wa Foundation for Civil Society wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Tafrija hiyo, Ambao pia ni wana AZAKI wanaofanyanao kazi kupitia miadi mbalimbali wanayoiendesha, leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad