BRELLA KUSAINI MOU NA TAMISEMI KWA AJILI KUSOGEZA HUDUMA ZA USAJILI KARIBU NA WANANCHI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 5 March 2019

BRELLA KUSAINI MOU NA TAMISEMI KWA AJILI KUSOGEZA HUDUMA ZA USAJILI KARIBU NA WANANCHI

NA TIGANYA VINCENT
WAKALA  wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELLA) inatarajia kuingia makubaliano na Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kwa ajili ya kuona jinsi ya kuwatumia Maafisa Biashara wa Halmashauri ili kusogeza karibu huduma za usajili wa majina na nembo za biashara kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa BRELLA Bakari Mketo wakati wa semina ya siku moja iliyowahusiasha Maafisa Biashara, Maendeleo ya Jamii, Wanasheria, , SIDO na TCCIA mkoani Tabora. Alisema lengo la BRELLA ni kumuondolea usumbufu mwananchi anayetaka kusajili jina la biashara na nembo ya biashara yake katika mazingira yaliyo karibu yake badala ya kusafiri kwenda Dar es salaam na wakati mwingine kukutana na vishoka ambapo wanamuibia fedha zake.

Mketo alisema wameamua kuangalia uwezekano wa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kuwa ziko karibu na wananchi wengi na baadhi ya shughuli za kila siku za Maafisa biashara ni pamoja na kukutana na wafanyabaishara. Alisema baadhi ya wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa wamekuwa hawanufaiki na kazi zao kwa sababu ya kushindwa kusajili na kuwa na nembo ya biashara zao.

Mketo alisema wanapotekea wajanja wachache wanatumia nembo zao ambao hazijasajiliwa kwenda kusajili na kisha waanzirishi kubaki maskini na kushindwa kisheria kwa sababu walichelewa kujisajili. Aidha alisema BRELLA pia imeanzisha mfumo mpya wa kusajili biashara na nembo za wafanyabiashara kupitia Mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao(ORS) ambapo mtu aweza kujisajili sehemu yoyote ambapo simu yake ina huduma ya  tovuti.

Alisema wameamua kutumia njia hiyo ili kupunguza urasimu kwa wananchi wa kuwataka kwenda Dar es salaam ndio wasajili nembo za biashara zao. Naye Afisa kutoka BRELLA Suzan Senso alisema ili mtu asajili nembo ya biashara yake atapaswa kuwa na kitambulisho cha Taifa.

Kwa upande wa Mfanyabisahara kutoka Sikonge Faibeti Michael alisema elimu waliyopatiwa itawasidia kulinda haki za nembo za biashara zao na pindi akitaka kuitumia itabidi alipwe na hivyo kunufaika. BRELLA watembelea maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuwaelimisha mfumo mpya wa usajili wa biashara na nembo.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Wakala  wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELLA)  Bakari Mketo akitoa elimu leo kwa Maafisa Biashara, Maendeleo ya Jamii, Wanasheria, , SIDO na TCCIA mkoani Tabora juu ya umuhimu wa kusajili majina ya biashara na nembo za biashara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad