HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 18 February 2019

Wema Sepetu afunguliwa rasmi na bodi ya filamu Na Khadija Seif , Globu ya Jamii
MSANII wa Bongomovie Wema Sepetu amefunguliwa rasmi na bodi ya filamu Tanzania kuendelea na kazi zake za filamu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Joyce Fissoo amesema Wema alifanya kosa la kusambaza picha jongevu ambayo ilikua ikikinzana na maadili ya kitanzania na kujisababishia bodi ya filamu kumfungia kwa muda usiojulikana.

Aidha Fissoo ameeleza kuwa kwa kipindi chote Wema Sepetu amekua akikiri kosa alilolifanya na kujutia  akiwa kama kioo cha jamii alipaswa kuifundisha jamii na sio kuvunja mila na desturi na tamaduni za kitanzania .

"Kwa kipindi chote bodi ya filamu ilimtaka wema kuandaa maandiko pamoja na kukutana na mashabiki zake na wasio shabiki zake ili kujitathimini nakupata taswira vile jamii inavyomchukulia na kuwasilisha kwa bodi ya filamu," alisema fissoo.

Fissoo ameeleza kuwa pamoja na adhabu waliyompa Wema Sepetu ameweza kubainisha changamoto alizozipata katika utayarishaji na uandaaji wa kazi zake ikiwemo filamu ya Superstar aliyomshirikisha msanii van Vicker kutoka nchi ya Nigeria kuwa pesa ilikua kikwazo katika uandaaji wa filamu hiyo.


"Tumejidhihirisha na kuamua kumfungulia wema sepetu kutokana na kukiri kubadilika na kufanya mapinduzi katika tasnia kwani Wema ni msanii mwenye mashabiki wengi nje na ndani ya nchi kwa umahiri wake wa uigizaji," alisema Fissoo.

Kwa upande wake muigizaji Wema Sepetu ameushukuru uongozi wa bodi ya filamu chini ya mama mlezi Joyce fissoo kwa kipindi chote alichokua akitumikia adhabu yake na kumfundisha maadili mazuri kwa jamii yake ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya tasnia kwa ujumla .

"Adhabu niliyopewa Mimi ikawe ndio fundisho kwa wasanii wengine kutorudia kitendo hicho cha uvunjifu wa maadili,"alisema wema

Pia Wema amesema anaimani na bodi ya filamu ipo kwa ajili ya kurekebisha kazi za sanaa pamoja na maadili na si kurudisha nyuma wasanii kimaendeleo na ni wakati sasa wa kujitambua na kujithamini  hususani wasanii wa kike na kujijengea heshima.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kumfungulia rasmi msaani wa filamu mchini Wema Sepetu aliyekua amefungiwa kwa muda usiojulikana. Kulia ni Msanii wa filamu, Wema Sepetu.
 Msanii wa filamu Tanzania,Wema  Sepetu akiishukuru bodi ya filamu kwa kumfungulia rasmi kuafanya kazi ya sanaa hapa nchini.(Picha na Emmanuel Maasaka,MMG)

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad