• Mtaa Kwa Mtaa TV
  • Michuzi Blog
  • Jiachie Blog
  • MK Computer Tweaks

MTAA KWA MTAA BLOG

test banner
    • Habari
    • Kimataifa
    • Biashara
    • Matukio Mtaani
    • Habari za Michezo
    • Burudani
    • Contact Us

    HABARI MPYA

    Home Top Ad

    Post Top Ad

    Saturday, February 2, 2019

    Home BURUDANI WASANII WA FILAMU NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA WALEDI NA UFANISI KWENYE KAZI ZAO

    WASANII WA FILAMU NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA WALEDI NA UFANISI KWENYE KAZI ZAO

    Othman Michuzi February 02, 2019 BURUDANI,
     KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu wa mkoa wa Tanga
     KATIBU Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo akizungumza katika mafunzo hayo
     KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Mathew Bicco akizungumza katika mafunzo hayo
      Mwezeshaji wa Mada ya Uandishi wa Miswada ya Filamu Dkt Richard Ndunguru kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu mkoani Tanga.
     Msanii nguli wa Filamu mkoani Tanga akizungumza wakati wa mafunzo hayo kulia ni KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala
     Sehemu ya wasanii wa filamu mkoani Tanga wakifuatilia mafunzo hayo
     Sehemu ya wasanii wa filamu mkoani Tanga wakiwa kwenye mafunzo hayo
    KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo kulia ni  KATIBU Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo kushoto ni nKATIBU Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Mathew Bicco
    WASANII wa filamu hapa nchini wametakiwa kuhakikisha wanazingatia waledi na ufanisi mkubwa kwenye kazi zao ili ziweze kuwa chachu ya maendeleo kwa jamii zinazowazunguka kutokana na tasnia hiyo hivi sasa kuwa mkombozi kwenye jamii.

    Hayo yalisemwa na Mwezeshaji wa Mwezeshaji wa Mada ya Uandishi wa Miswada ya Filamu Dkt Richard Ndunguru kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu mkoani Tanga.

    Alisema kwamba sanaa inaweza kuwa tija kubwa ya maendeleo kwa wasanii kwa kutengeneza ajira nyingi na kuweza kuwakomboa iwapo wataizingatia na kuithamini kwa kuonyesha walezi kwenye kazi zao.

    “Ndugu zangu wasanii labda niwaambie kwamba mkiwa makini kwenye kazi zenu na kuzingatia weledi mkubwa mnaweza kufika mbali kimafanikio kutokana na namna tasnia ya filamu hapa nchini iliyokuwa”Alisema.

    Aidha alisema pia wasanii lazima watambue kwamba hawawezi kutengeneza filamu nzuri kama hawatakuwa na muda wa kutazama wenzao wanafanya nini kwani kupitia wenzao wanaweza kujifunza na kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa”Alisema.

    “Labda pia niwaambie kwamba waledi kwenye kazi ya sanaa ni kitu muhimu sana inaweza kukupa maendelea makubwa kwa kuhakikisha mnaipenda na kuithamini “Alisema .

    Naye kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fisso alisema sekta ya filamu ni ya kiuchumi kutoka Tanzania ni ya pili kwa idadi uzalishaji ukilinganisha na nchi ya Nigeria lakini ukija kwenye pato la Taifa kidogo wanahitaji kuongeza nguvu.

    Alisema bodi ya filamu imeweka mpango mahususi wa kuwajengea uwezo wadau wa filamu hapa nchini hususani kwenye maeneo ya kuboresha kazi zao ili ziwe kuwa na tija.

    Aidha alisema hilo linatokana na baadhi ya wasanii hususani wanaochipukia kutokutambua namna ya kuweza kutengeneza kazi zao na kuweza kuzitangaza ili ziweze kuwa na manufaa makubwa kwao.


    Mwisho



















    Tags # BURUDANI
    Mtumie Rafiki Yako
    BURUDANI
    Posted by Othman Michuzi at February 02, 2019
    Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
    Labels: BURUDANI

    No comments:

    Post a Comment

    Newer Post Older Post Home
    Subscribe to: Post Comments (Atom)

    Post Bottom Ad

    OTHMAN MICHUZI

    Facebook

    Recent

    ZILIZOSOMWA ZAIDI

    • Wild Corrida Slot, Ijaribu Bure kwenye Meridianbet
      Wild Corrida Slot, Ijaribu Bure kwenye Meridianbet
        Unataka kutembea kwenye viatu vya bullfighter? Jaribu slot ya mtandaoni ya Wild Corrida kutoka Expanse Studios na utakuwa ukimsaidia wild...
    • Sababu Kumi za Kujaribu Casino Heist ya Meridianbet,Sherehe ya Ushindi imeanza
      Sababu Kumi za Kujaribu Casino Heist ya Meridianbet,Sherehe ya Ushindi imeanza
      MERIDIANBET  inakuletea toleo jingine makini la msisimko wa Casino katika mchezo wa CASINO HEIST-na hii sio sloti ya kawaida tu. Kila...
    • ACHIA NGAZI BIBI MCHUMA UNAONDOKA HUOOOO.....
      ACHIA NGAZI BIBI MCHUMA UNAONDOKA HUOOOO.....
    • MFAHAMU MISS TANGA 2001 ALIYEJIKITA KATIKA KUSAIDIA JAMII
      MFAHAMU MISS TANGA 2001 ALIYEJIKITA KATIKA KUSAIDIA JAMII
        Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii KAMA Mwanamke ukiamua kujitoa na kupigania nini unafanya lazima utafanikiwa, nami naweza kuse...
    •  TANZANIA YAFAFANUA UMOJA WA MATAIFA KUWA HAINA ARDHI YA MAKABILA
      TANZANIA YAFAFANUA UMOJA WA MATAIFA KUWA HAINA ARDHI YA MAKABILA
      Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Tanzania Profesa Hamis Malebo akiwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa u unaondelea New York ,Mar...

    MAONI

    KUMBUKUMBU

    MTAA KWA MTAA TV

    MIAKA 60 YA MUUNGANO

    Mac Auto Accessories

    TWEAKED BY:

    HARUSI

    KAMERA YA MTAA KWA MTAA

    KIMATAIFA

    Contact Form

    Name

    Email *

    Message *

    Crafted with by TemplatesYard
    MTAA KWA MTAA BLOG © 2024. All Rights Reserved.
    Developed by MKCT