Na Sophia Mtakasimba , Bagamoyo
WAUMINI wa kanisa la Waadventista Wasabato Bagamoyo
wametakiwa kufanya kazi ya kushirikiana ili kuweza kusaidia kazi ya Mungu
kusonga mbele na kuwafikia watu wengi.
Wito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Jimbo la Mashariki kati mwa Tanzania , Mchungaji Joseph Mngwabi ambaye
alikuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa
Kanisa jipya la kisasa la Waadiventista wasabato Bagamoyo uliofanyika jana
(jumamosi) wilayani Bagamoyo mkoani Pwani .
“Mkifanya kazi kwa kushirikiana na kwa lengo moja
,mtafanikiwa sana kufikia malengo mliyojiwekea na hii itasaidia sana kufanya
kazi ya Mungu isonge mbele”alisema Mchungaji Mngwabi.
Awali katika hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi Mchungaji wa
mtaa wa Bagamoyo Mch.Melkizedeki Wanjala, alisema kuwa kanisa la Waadventista
Wasabato Bagamoyo lilitengwa kuwa Kanisa kutoka Kanisa mama la Mwenge mnamo mwaka 1995,ambapo hadi kufika mwaka 2001 Kanisa lilifanikiwa kuwa wa jengo lake la
kuabudia eneo la Tandika-Bagamoyo. Lakini kufikia mwaka 2013 idadi kubwa ya waumini
iliongezeka,hali hii ilipelekea jengo la awali kutotosha ,hivyo kuwa na hitaji
la kuwa na Kanisa kubwa zaidi.
Akizungumzia ujenzi wa jengo jipya la Kanisa Mchungaji
Wanjara amesema kuwa jengo hilo litagharimu jumla ya Shilingi za kitanzania
Milioni Mia Nne na Hamsini (450,000,000) hadi kukamilika kwake ,hivyo amewataka
washiriki kushirikiana kwa hali na mali ili kukamilisha ujenzi huo huku akinukuu
Maandiko Matakatifu kutoka kitabu cha Kutoka 25:8 yanayosema “nao wanifanyie
patakatifu ili nipate kukaa kati yao.
Askofu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo la Mashriki
Kati mwa Tanzania ,Mchungaji Joseph Ngwambi(Kushoto) , akiweka jiwe la msingi
katika ujenzi wa kanisa la Waadventista wa Sabato Bagamoyo, Kulia ni wa Jimbo la
mashariki kati mwa Tanzania Ndg.Enock Rabieth .
No comments:
Post a Comment