HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 5 February 2019

WAFANYABIASHARA, WAGANGA WA JADI WAKAMATWA NJOMBE MAUAJI YA WATOTO

Baadhi ya waganga wa kienyeji wa Njombe walikutana wa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni wiki iliyopita.


Wafanyabiashara 10 mashuhuri ni miongoni mwa washukiwa 28 waliyokamatwa kuhusiana na mauaji ya kikatili ya watoto katika eneo la Njombe Tanzania.

Mbunge wa Mkambako Deo Sanga, ameliambia bunge kuwa hali ya taharuki imetanda katika eneo hilo kiasi cha kuwa wageni wanachukuliwa kama washukiwa au washirika wa karibu wa wauaji.

''Karibu wafanyibiashara 10 ambao wamewaajiri watu 200 wamekamatwa siku nne zilizopita na hatujui kinachoendelea kufikia sasa'' alisema Mbunge Deo Sanga kama alivyonukuliwa na Gazeti la kingereza la The Citizen la Tanzania akiongezea kuwa shughuli za kiuchumi katika eneo hilo zimekwama.

Bw. Sanga alikua akichangia hoja iliyotolewa na mbunge mwenzake wa Lupembe Joram Hongole aliye muomba spika Job Ndugai kuahirisha shughuli za siku ilikujadili suala la mauaji ya watoto mkoani Njombe.

Mamlaka za eneo hilo zinasema kuwa takribani watoto 10 wameuawa Njombe katika kipindi cha mwezi mmoja na kwamba wauaji wamekuwa wakiwakata wathiriwa viungo vya mwili kama macho, meno na kunyofoa sehemu zao za siri.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mauaji ya watoto hao sita wilayani humo yalichochewa na imani za kishirikina.

Waganga wa tiba za jadi wilayani Njombe hata hivyo wamejitenga na tuhuma kuwa wanachochea mauaji ya watoto wilayani humo.


Akithibitisha kukamatwa kwa washukiwa 28,kamanda wa polisi katika eneo la Njombe Bi Renata Mzinga ameongeza kuwa shughuli ya kuwasaka washukiwa zaidi wa mauaji hayo inaendelea.''Tumevumbua mtandao wa watu waliyohusika na mauaji hayo.Tunashirikiana na kitengo maalum cha polisi kutoka makao makuu ya polisi mjini Dar es Salaam kuhakikisaha wote waliyohusika na ukatili huo wanatiwa nguvuni'' alisema Bi Renata.


Spika wa bunge Job Ndugai ameipatia serikali hadi Ijumaa ya Februari 8 kutoa taarifa kamili kuhusiana na matukio mkoani Njombe. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad