HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 11, 2019

UVCCM MKOA WA PWANI YATOA MAFUNZO YA UJASILIAMALI WILAYA YA KISARAWE

Umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa pwani umeendelea kutoa mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana na wananchi wa Kisarawe yaliyoyofunguliwa jana na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

Akifungua Mafunzo hayo DC Jokate amesisitiza vijana kuchangamkia FURSA na amewapongeza Uvccm Mkoa wa Pwani kwa kuandaa Mafunzo hayo katika wilaya hiyo.

DC Jokate ameahidi kuwapa ushirikiano washiriki wa mafunzo hayo na amesema wajasiliamali wajitume kufanya kazi kwa maendeleo ya kisarawe.

"Niwasihi Vijana Wenzangu Mjikite kwenye Ujasiliamali wa Kilimo ambapo kwa ardhi ya wilaya yetu inakubali nasi viongozi wenu tutahakikisha tunawatafutia soko la uhakika na wadau wa kilimo hicho;

"Kwa Sasa wilaya yetu tunafanya vizuri Sana katika sekta mbalimbali mfano nilipokuja hapa wilaya nzima matokeo ya kidato cha nne daraja la kwanza wanafunzi walikuwa wanatoka 4 tu Ila kwa kampeni yetu ya Tokomeza Zero Kisarawe Imesaidia kwa Sasa wanafunzi 41" Alisema DC Jokate.

Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Pwani Cde Charangwa Selemani, amesema mafunzo hayo ni muendelezo wa kuwapa vijana ujuzi katika wilaya zote za Mkoa wa pwani na mpaka sasa wameshafanya wilaya mbili ikiwemo RUFIJI na KISARAWE. 

Aidha Mwenyekiti Charangwa amesisitiza umoja na mshikamano katika kazi na wao kama viongozi watahakikisha wanawapa vijana ujuzi Ili waweze kujiajiri.

Comrade Charangwa amewapongeza Viongozi wa Chama na serikali kwa Uchapakazi na amempongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Joseph Pombe Magufuli, kwa kazi kubwa anayoifanya kwa Watanzania.

"Mwaka Huu Kuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vijana Ndo Injini ya Chama Shirikianeni na Chama Kuhakikisha Wilaya ya Kisarawe Tunapata Ushindi wa Kishindo pia Mafunzo Haya Myafanyie Kazi Tengenezeni Bidhaa za Ushindani katika Soko" Alisema Cde Chalangwa.

Katika mafunzo hayo Mwenyekiti wa Uvccm Wilaya ya Kisarawe,Asha Lusonzo, Amemshukuru mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa pwani kwa namna anavyoshirikiana nao katika kuwapelekea fursa na wameahidi kuzifanyia kazi.

mafunzo hayo ya ujasiliamali yalihudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Mkoa wa Pwani,Abdallah Makelo, Katibu Msaidizi wa Mwenyekiti Taifa, Abdulrahaman Killo, Katibu wa Uvccm Mkoa wa Pwani,Ramadhan Kapeto, Viongozi wa UWT wilaya ya Kisarawe, viongozi wa jumuiya ya wazazi wilaya kisarawe,Katibu Uvccm wilaya kisarawe, waheshimiwa madiwani , DAS wa wilaya ya kisarawe,afisa maendeleo wa wilaya na afisa vijana wa wilaya.

Vijana wa Wilaya ya kisarawe walijifunza mambo mbalimbali ikiwemo Kilimo ,Ufugaji wa Kuku,Uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani Mafunzo yaliyo tolewa na Taasisi ya TAEDO chini ya Mkurugenzi wake Kenani Kihongosi.

Mafunzo hayo yalifungwa na mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Kigoma,Cde Silvia Sigula ambaye aliwaasa vijana kutumia fursa zilizopo na kufanyia kazi mafunzo waliyopewa katika kujiongezea kipatao chao.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (katikati) akifungua Mafunzo ya Ujasiliamali kwa Vijana wa wilaya hiyo  yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi. Mafunzo Hayo yameandaliwa na Taasisi ya Taedo na Uvccm Mkoa wa Pwani. Kulia Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Pwani, Chalangwa Seleman na Mwenyekiti Uvccm Wilaya ya Kisarawe,Asha Lusonzo. 
 Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Pwani, Chalangwa Seleman (katikati) akichanganya dawa kwenye maji wakati wa mafunzo ya Ujasiliamali wa vitu mbalimbali wilayani Kisarawe jana. Wa Kwanza Kushoto ni Mwenyekuti wa Uvccm wa Wilaya ya Kisarawe,Asha Lusonzo. 
 
 Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (Uvccm), Chalangwa Selemani akizungumza katika Mafunzo ya Ujasiliamali kwa Vijana wilayani Kisarawe, kushoto ni Mkuu wa Wilaya Hiyo, Jokate Mwegelo.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad