HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 22 February 2019

Tanzania imeingia orodha ya 27 Duniani katika ubunifu - HDIF


Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
KUTOKANA na maendeleo ya uvumbuzi nchini, Tanzania imeshika nafasi ya 27 katika orodha ya ubunifu duniani kutoka nafasi ya 123 mwaka 2013 hadi 92 mwaka huu. Sababu zilizochangia Tanzania kufikia hatua hiyo ni kuanzishwa kwa vituo vipya vya teknolojia, ongezeko la ufahamu juu ya uwezo wa ubunifu katika kutatua changamoto kubwa za kimaendeleo.

Hayo yalibainishwa leo Februari 22, 2019 jijini Dar es Salaam na Kiongozi wa  Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Binadamu (HDIF), David McGinty wakati wa uzinduzi wa ripoti  inayojulikana kwa jina la 'Kuwekeza katika ubunifu na Teknolojia nchini Tanzania-Fikra na Mapendekezo ya HDIF 2013-2018'.
McGinty amesema kuwa zaidi ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa mfuko huo, wamesaidia wavumbuzi wengi nchini ili kutekeleza mawazo yao kwa ufanisi na kuwapa mbinu mpya za kutimiza malengo. Amesema kuwa HDIF imekuwa bingwa wa kuvumbua vipaji vya baadhi ya Watanzania wenye ubunifu mkubwa na mashirika ambao wamewekeza nguvu na rasilimali nyingi kushughulikia changamoto za maendeleo nchini.

"Ingawa Tanzania mazingira ya kukuza ubunifu bado yako katika hatua za awali, taasisi zinazoshughulika na ubunifu, zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uchache wa rasilimali na vipaumbele katika mashindano," amesema McGinty. Amesema ripoti hiyo inalenga kuleta kichocheo cha mabadiliko kwa kuongeza ujuzi na ufahamu kuhusu ubunifu katika jamii, pia kuongeza ufahamu wa HDIF juu ya  kuboresha matumizi, viwango, uchukuzi wa ubunifu nchini.

"Ili kuendeleza upatikanaji wa huduma za msingi na kuimarisha mazingira ya ubunifu nchini. HDIF tunaomba mashirika mengine kutafakari njia zinazoweza kutumikia kusaidia kuchochea uvumbuzi ambao utaleta kabadiliko halisi na ya kudumu," alisisitiza.

McGinty ameeleza kuwa katika miaka mitano ya utekelezaji wa mfuko huo, wamekutana na changamoto mbalimbali zilizosababisha mikakati iliyopangwa kutofanikiwa kwa ufanisi na kwamba HDIF inatarajia kubadilishana uzoefu na washirika wengine katika kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumiwa kwa ufanisi na kuchagua njia bora.

Kwa upande wake,  Naibu Kiongozi wa HDIF, Joseph Manirakiza   amesema fursa ya kuinua masuala ya ubunifu Tanzania yamesaidia kuvutia baadhi ya wafadhili wa kimataifa na wawekezaji.
Amesema HDIF inahamasisha ushirikiano kati ya wadau katika kuongeza kubadilishana taarifa ya mambo waliyojifunza ikiwemo changamoto.

"HDIF inatarajia kukamilisha kazi yake mwaka 2021 lakini kwa wakati wote miradi itaendelea kuwa kielelezo cha ubunifu nchini," amesema Manirakiza. Ameongeza kuwa  katika miradi mbalimbali ambayo waliifadhili imeleta matokeo chanya ikiwemo  mradi wa maji unaotumia mfumo wa malipo kabla uliopo Karatu mkoani Arusha.

Ameeleza kuwa mafanikio waliyoyapata yanayotakana na ushirikiano wa wadau wa masuala ya ubunifu ikiwemo Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), vyuo vikuu  na wanafunzi.
 Kiongozi wa mfuko wa Ubunifu na Maendeleo (HDIF)  David McGinty akizungumza na wanahanabri pamoja na wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari wakati wa uzinduzi wa kupitia nanayojulikana kwa jina la 'Kuwekeza katika ubunifu na Teknolojia nchini Tanzania-Fikra na Mapendekezo ya HDIF 2013-2018', uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
 Naibu Kiongozi wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya watu (HDIF), Joseph Manirakiza akizungumzia miradi waliyoitekeleza kwa miaka mitano (mwenye shati la mistari). Wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo,jijini Dar es Salaam
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya watu (HDIF), Hannah Mwandoloma akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti  inanayojulikana kwa jina la 'Kuwekeza katika ubunifu na Teknolojia nchini Tanzania-Fikra na Mapendekezo ya HDIF 2013-2018', uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
 Mchora Vobonzo Masoud Ally 'Kipanya' akiongoza mjadala kuhusu mchango wa waandishi wa habari katika masuala ya ubunifu baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo, jijini Dar es Salaam. Pombeni yake ni  baadhi wa wahariri kutoka vyombo vya habari. 

 Baadhi ya wadau wa habari wakichangia mada wakati wa uzinduzi wa kupitia nanayojulikana kwa jina la 'Kuwekeza katika ubunifu na Teknolojia nchini Tanzania-Fikra na Mapendekezo ya HDIF 2013-2018', uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
 


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad