HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 6 February 2019

STARTIMES YAANDA SHINDANO LA WAPENDANAO

KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd leo imetangaza kuanza msimu mpya wa burudani kupitia chaneli mbali mbali ndani ya king’amuzi chake cha StarTimes. Katika msimu huo mpya wa burudani kutakuwa na maudhui tofauti  kuanzia tamthiliya mpya, michezo pamoja na vipindi vipya vya Burudani na hiyo ni kwa  mwezi huu wa wapendanao ambapo StarTimes pia wameleta shindano kupitia akaunti zao za mitandao ya Kijamii za facebook na Instagram.

Akizungumza na  wanahabari Meneja Masoko wa Startimes Davis Malisa amesema kuwa, "Kuna nafasi ya kujishindia vifurushi vya juu kabisa kwa watu 10, ila zawadi kwa couples mbili ambao simulizi zao zitakuwa nzuri zaidi, watapata zawadi ya kulala Siku moja katika hoteli ya Slipway, Masaki iliyopo kwenye Ufukwe wa bahari, na watagharamiwa vyakula pamoja na vinywaji kwa siku nzima”. Amesema Malisa.

Kwa upande wake Afisa Mahusiano wa StarTimes Sam Gisayi amesema kuwa katika kuhakikisha wateja wao wanapata burudani wanayostahili, StarTimes kupitia chaneli ya ST Swahili wataanza kuonyesha msimu mpya wa Coke Studio Africa kuanzia jumapili hii tarehe 10 Februari. Kipindi cha Coke Studio Africa ni moja ya vipindi vya Burudani vinavyopendwa zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Amesema kuwa, "Tunazidi kujipambanua kama Wafalme wa burudani za familia, na Coke Studio Africa ni kipindi kinachoweza kuangaliwa na familia nzima, muziki wa kuvutia ambao haupatikani sehemu nyingine" ameeleza.

 Amesema kuwa Coke Studio Africa kwa mwaka huu wasanii watano kutoka Tanzania wanaofanya  wanafanya vizuri ndani na nje ya mipaka ya Tanzania watakuwemo na hao ni pamoja na Nandy, Harmonize na Rayvanny kutoka WCB, JUX na Mimi Mars.

Mbali na Coke Studio Afrika StarTimes wameandaa burudani zikiwemo tamthiliya pamoja na ligi ya Uingereza kupitia ST World.
 Meneja Masoko wa StarTimes, David Malisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimu mpya wa burudani kupitia chaneli mbalimbali ndani ya king’amuzi chake cha StarTimes leo jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Mahusiano StarTimes, Samwel Gisayi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyojipanga kuboresha huduma zao kwenye msimu mpya wa burudani kupitia chaneli mbalimbali ndani ya king’amuzi chake cha StarTimes leo jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad