HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 19 February 2019

SIMBA VITANI KUIKABILI AFRICAN LYON LEO


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) Simba inashuka dimbani leo kucheza na African Lyon Jijini Arusha.Mchezo huo ni muendelezo wa. Ligi Kuu na utakuwa mchezo wake wa 17 wa Ligi utapigwa kwene dimba la Shekhe Amri Abeid kuanzia sa 10 alasiri.

Simba watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kutoka kuwafunga watani wao wa jadi Yanga kwenye mchezo wa ligi uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Ofisa habari ww Simba Hajji Manara amesema kikosi kimejiaandaa kwa ajili ya mchezo huo na matumaini makubwa ni kuona wanaweza kupata alama tatu ugenini.

"Tunawaheshimu African Lyon ni timu nzuri, ila nasi pia hatuna budi kufanya kile ambacho mashabiki wanahitaji, tayari wachezaji na uongozi umeweza kuimudu hali ya hewa ya huku Arusha, ni wakati tu, sapoti ya mashabiki pamoja na dua ni vitu muhimu," amesema Manara.

Timu hiyo yenye alama 39 wakiwa nafasi ya tatu ya Ligi inatarajia kuwakosa wachezaji wake wa kimataifa Meddie Kagere na Emanuel Okwi. Baada ya mchezo huo, Simba waterejea Jijini Dar es Salaam kuvaana na Azam Fc ikiwa ni mchezo wa kiporo wa mzunguko wa kwanza wa TPL.

Mechi zingine za Ligi ni Coastal Union wakiwa nyumbani wakiwakaribisha Azam Fc, Mwadui akicheza na Biashara United pamoja na Kagera akicheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mlandizi.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad