HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 5, 2019

SERIKALI YA DRC YATETEA MAWAZIRI KULIPWA MAISHA YAO YOTE

Waziri mkuu anayeondoka Bruno Tshibala alisaini maagizo hayo mnamo Novemba. Haki miliki ya picha GETTY IMAGES

Serikali ya Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo imetetea maagizo yanayoruhusu mawaziri kulipwa mishahara na marupurupu kwa maisha yao yote.


Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, serikali imesema malipo hayo "sio ya kuwatajirisha maafisa".
Maagizo mawili, yanayoruhusu mawaziri kupokea marupurupu ya kiwango cha chini zaidi $2,000 yameshutumiwa pakubwa.

Idadi kubwa ya raia nchini Congo wanaishi katika umaskini.

Serikali inayoondoka ilikuwa inawapatia mawaziri "kiwango cha chini kuwatosheleza mahitaji yao ya kimsingi, kama chakula, makaazi na huduma ya afya".

Malipo hayo "ni ya kuwaepusha kuishia katika umaskini", taarifa inasema.

Maagizo hayo mawili, yaliotiwa saini na waziri mkuu anayeondoka Bruno Tshibala mnamo Novemba, yaliripotiwa pakubwa hivi karibuni tu katika vyombo vya habari.

Agizo la kwanza linawapa mawaziri wakuu mishahara ya kila mwezi yalio sawa na 30% ya mshahara anaopokea sasa waziri mkuu, tiketi ya mara moja ya ndege kwa mwaka na marupurupu ya nyumba yenye thamani ya $5,000, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Agizo la pili linawapa mawaziri mishahara sawa na 30% ya mawaziri wa sasa na $1,000 kila mwezi kulipia makaazi. Watapokea pia tiketi ya mara moja kwa mwaka ya ndege, Reuters linaripoti.Haki miliki ya picha REUTERS

Maagizo hayo yalishutumiwa pakubwa katika nyanja zote kisiasa.
Mshauri wa rais wa zamani Joseph Kabila amesema "hayaendani na mtazamo wetu wa kiuchumi na kijamii".

Patrick Nkanga ameandika kwenye Twitter: "Ni kupita kiasi na ni gharama kubwa zisizohitajika kwa fedha za umma." Lakini serikali imetetea maagizo hayo na kueleza kwamba hayatozingatia mawaziri wa awamu iliopita, badala yake ni kwa walioko kwenye serikali ya sasa na serikali zijazo.

Rais mpya wa Jamhuri ya Kidmeorasi ya Congo, Felix Tshisekedi, aliapishwa madarakani mwezi uliopita. Alipokea wadhifa huo kutoka kwa Kabila katika ukabidhi wa kwanza wa madaraka uliofanyika kwa amani katika nchi hiyo na uliowahi kushuhudiwa katika miaka 60.

Matokeo ya uchaguzi yalishutumiwa pakubwa, huku kukiwa na ripoti za makubaliano kati ya rais Kabila na bwana Tshisekedi -hatahivyo pande zote zilikana tuhuma hizo.
Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad