HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 6 February 2019

SAFARI ZA NDEGE KWENDA DODOMA KUANZA APRILI MOSI MWAKA HUU- PRECISION AIR

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Shirika la ndege la Precision Air limetangaza  rasmi kuanza kwa safari za ndege  kati ya Dar es Saalaam – Dodoma na Kiilimaanjaaro-Dodoma kuanzia tarehe 1, Aprili 2019.

Meneja Masoko na Mahusiano wa Shirika hilo, Hillary Mremi, amesema kwamba Precision Air itakua ikafanya safari sita kwa wiki kuelekea Dodoma kati ya siku za Jumatatu,Jumanne,Jumatano, Alhamisi,Ijumaa na Jumamosi.

Amesema kuwa, katika siku za Jumatano na Ijumaa safari za Dodoma zitakua zikipitia Kilimanjaro na kwa siku zilizobakia safari ziatakua ni za moja kwa moja.

“Safari zetu hizi mpya zitaiiunganisha Dodoma na mikoa mingine kama Mtwara, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Nairobi kupitia Dar es Salaam na Kilimanjaro. Abiria kutoka maeneo haya wataweza kuunganisha safari zao kuelekea Dodoma kupitia mtandao wetu wa safari, na hivyo kuunganisha jamii jambo ambalo ni moja kati ya malengo yetu makuu.” alisema Mremi.

Mremi ameeleza zaidi kuwa kwa safari za moja kwa moja Ndege itakua ikiondoka Dar es Salaam saa 3:15 Asubuhi na kufika Dodoma saa 4:20 Asubuhi, huku kwa safari za kupitia Kilimanjaro Ndege itakua ikondoka Dar es Salaam saa 8:00 Mchana na kufika Dodoma saa 10:15 Mchana.

Amesema kwa safari za moja kwa moja kutokea Dodoma, Ndege itakua ikiondoka saa 4:45 Asubuhi na kufika Dar es Salaam saa 5:50 Asubuhi, huku kwa safari za kuptia Kilimanjaro Ndege itakua ikiondoka saa 11:15 Jioni na kuwasili Kilimanjaro saa 12:15 Jioni na Dar es Salaam saa 2:05 usiku.

Shirika hilo lilitangaza kuanza kwa safari za ndege kuelekea Jiji la Dodoma ikiwa ni katika kurahisisha usafiri kwa watendaji wa serikali baada ya Makao Makuu ya nchi kuhamia rasmi kwenye Jiji hilo.
Meneja Masoko na Mahusiano wa ShiShirika la ndege la Precision AirHillary Mremi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad