HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 8 February 2019

RC TABORA ATOA MWEZI MMOJA KWA MA DC NA MADED MKOANI HUMO KUHAKIKISHA VITAMBULISHO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO VINAKWISHA

Na Tiganya Vincent
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa mwezi mmoja kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wote kuhakikisha zoezi la utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo linakamilika. Hatua hiyi imefikiwa baada ya kuona utekelezaji wa zoezi hilo unasua sua kwani hadi sasa ni vitambulisho elfu saba tu vilivyogawiwa kati ya elfu 25 vya awamu ya kwanza.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akikabidhi vitambulisho vingine elfu 40 kwa  Halmashauri  nane za Mkoa huo.   Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo ndicho kitakuwa kipimo cha utendaji kazi wao.

Alisema hatawavumilia watendaji hao watakaoshindwa kukamilisha zopezi hilo katika muda waliokubaliana na kuongeza Mtendaji atakayeshinwa atawajibishwa kwa kushindwa kutekeleza agizo wa Rais. Mwanri aliwaagiza Wakuu wa Wilaya zote mkoani humo kuongeza kasi ya ufuatiliaji ili wafanyabiashara wadogo wachukue vitambulisho hivyo na waweze kufanya biashara zao wakiwa uhuru.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema  zoezi la utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo hadi sasa ni asilimia 28 tu ndo vimegawiwa. Alisema kuwa hadi Februari 7 mwaka huu ni vitambulisho 7,013 ndivyo vilivyokwisha gawiwa kwa wafanyabiashara hao kati vitambulisho 25 elfu vilivyopokelewa  awamu ya kwanza.

Makungu alisema kwamba kiasi cha fedha kilichokusnywa kutokana na gharama za uchangiaji wa vitambulisho hivyo ni shilingi milioni 140.2 na zilizokwisha pelekwa mamlaka ya mapato ni milioni 135.9. Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(Uyui) ndiyo inaongoza kwa kugawa vitambulisho vingi kwa wafanyabiashara wadogo kwani hadi sasa imegawa 2,529 kati ya 3125 ilvyopewa awamu ya kwanza.

Makungu alisema kuwa Desemba 19 mwaka jana kila Halmashauri ilipewa vitambulisho 3,125 kwa ajili ya wafanyabiashara hao lakini  baadhi yake zimegawa chini ya asilimia kumi hadi sasa wakati wahusika wapo. Katibu Tawala huyo Mkoa alisema Manispaa ya Tabora ndiyo imegawa vitambulisho vichache kwa wafanyabiashara hao kwani hadi sasa waliopata ni 150 sawa na asilima tano tangu zoezi hilo lilipoanza mwishoni mwa mwaka jana.
 Baadhi ya watendaji kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Tabora wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa ajili ya wajasiriamali leo.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa taarifa fupi ya idadi ya vitambulisho ambavyo vimeshagawiwa kwa wajasiriamali hadi kufikia leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa maagizo leo kwa Watendaji wa Wilaya zote  ya kuhakikisha vitambulisho vyote vya wafanyabaishara ndogo ndogo viwe vimeshamalizika ifikapo Machi 8. 
 Wakuu wa Wilaya ya Mkoa wa Tabora( walio mstari wa mbele) wakisikiliza kwa makini maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha ) leo yakuwataka  kuhakikisha vitambulisho vyote vya wafanyabaishara ndogo ndogo viwe vimeshamalizika ifikapo Machi 8.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 5,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo(kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 5,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama (kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 10,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Godfrey Ngupula (kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo katika Halmashauri zake mbili za Wilaya hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 5,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri(kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 5,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya (kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 5,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa  (kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo. Picha na Tiganya Vincent

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad