HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 21 February 2019

RAIS DKT. SHEIN AFUNGUA JENGO LA SKULI YA SEKONDARI YA MICHEZANI PEMBA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar amesema kuwa siasa za vyama vingi zimekuja kwa lengo la kushidana kwa Sera na sio kukashifiana. 

Rais Dk. Shein aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa CCM wa Wilaya ya Mkoani Pemba pamoja na kufanya Majumuisho ya ziara yake kwa Wilaya hiyo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohamed Juma Pindua, iliyopo Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba ambapo viongozi kadhaa walihudhuria akiwemo Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.

Katika hotuba yake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais Dk. Shein alisema kuwa siasa za vyama vingi havikuja kwa lengo baya la kukashifana na badala yake vina lengo zuri la kushindana kwa Sera ili iwe kivutio kwa wanachama na sio ugomvi.

Hivyo, Rais Dk. Shein aliwasisitiza wananchi wa Wilaya hiyo kuishi kwa mapenzi na kufahamiana sambamba na kushirikiana pamoja kwao wote ni ndugu.

Aidha, Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliwataka viongozi wa CCM kutembelea Matawi, Wadi, Majimbo na Wilaya zao sambamba kuwatembelea wananchi na wanachama wa chama chao ili kuwasikiliza changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi.

Pia, Rais Dk. Shein aliwataka viongozi wa CCM wa Wilaya hiyo kuimarisha miradi ya ili chama hicho kiweze kupata mapato ya kuweza kukiimarisha na kuapata mafanikio makubwa zaidi.

Rais Dk. Shein alieleza kuwa tayari utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020 imeshatekelezwa kwa kiasi kikubwa na ahadi nyingi zilizoahidiwa zimeshatekelezwa sambamba na zile ambazo haziko katika Ilani.

Alisisitiza kuwa viongozi wote waliomo Serikalini ni vyema wakatambua kuwa wanatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha CCM, hivyo, wanakila sababu kufanya kazi zao kwa bidii na yule ambaye hatoweza anapaswa kukaa pembeni.

Aliongeza kwua huo ni utaratibu wa Serikali zote duniani kwa chama kinachoongoza Serikali  ni lazima viongozi wote watekeleze Ilani ya Chama hicho kwani ndicho kilicho madarakani na ndicho kinachoongoza nchi.

Rais Dk. Shein alieleza kuwa huo ndio utaratibu wa kimataifa na demokrasia ya nchi hivyo viongozi wote waliomadarakani katika Serikali anayoiongoza hawana budi kutekeleza Ilani ya CCM kwani ndicho chama kilicho madarakani,

Alieleza kuwa ujenzi wa  barabara ya Mkanyageni- Kangani (Km 6.5) ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 ambayo imetajwa katika Ilani hiyo kwenye ukurasa wa 149.

Aidha, ujenzi wa jengo la skuli ya Sekondari Michenzani, Mkoani Pemba pia ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi katika kuimarisha sekta ya elimu Zanzibar.

Ambapo pia, Rais Dk. Shein alieleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya CCM ya kujenga barabara ya Chake hadi Mkoani yenye (Km 27), ambayo hivi sasa imo katika mchakato wa michoro.

Rais Dk. Shein pia, aliusisitiza uongozi wa CCM wa Mkoa na Wilaya hiyo kuimarisha historia ya ASP kwa kulijenga jengo la Tawi la CCM lenye historia ya ASP huko Mkanyageni ambalo lilitumika na wazee waasisi kama vile marehemu mzee Mohamed Juma Pindua na yeye kuahidi kuchangia mabati kwa ajili ya ujenzi huo.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alizipongeza taarifa zilizotolewa mbele yake ikiwemo taarifa ya Serikali ya Wilaya ya Mkoani pamoja na taarifa ya Chama iliyotolewa na uongozi wa CCM Wilaya ya Mkoano.

Rais Dk. Shein pia, aliupongeza uongozi wa CCM Wilaya hiyo ya Mkoani kwa kuongeza idadi ya wanachama sambamba na ulipaji wa ada kwa wanachama wa chama hicho.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, na Mama Mwanamwema Shein, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri, wakiwa katika moja ya madarasa ya Skuli hiyo ya Sekondari ya Michezani baada ya ufunguzi wake ,likiwa na meza na viti vipya vilivyoagizwa na Serikali kwa Skuli za Sekondari na Msingi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati hafla ya Uzinduzi wa Madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Michezani Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba, akiwa katika ziara yake kutembelea Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba kuangalia miradi ya Maendeleo.(Picha na Ikulu)
 NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Bi. Madina Mjaka, akitowa Taarifa ya Kitaalam ya ujenzi wa Madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Michezani Wilaya ya Mkoani Pemba wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi leo.(Picha na Ikulu)
 /WANAFUNZI wa Skuli ya Michezani Wilaya ya Mkoani Pemba wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein. hayuko picha wakati wa hafla ya uzinduzi wa Skuli ya Sekondari ya Michezani leo, 21-2-2019.(Picha na Ikulu)

 WANANCHI wa Kijiji cha Michezani Wilaya ya Mkoani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi Skuli ya Sekondari ya Michezani Pemba.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimpongeza Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Michezo baada ya kumaliza kusoma Quran Surat Afaq Mwanafunzi Salim Shehe Hussein, kulia kwa Rais Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya Viti na Meza Mpya vilivyoagizwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ajili ya Skuli za Sekondari na Msingi Zanzibar, tayari vimeshagawiwa kwa Skuli za Sekondari za Unguja na Pemba, kwa ajili ya matumizi ya Wanafunzi.(Picha na Ikulu)
 JENGO Jipya la Skuli ya Sekondari ya Michezani Kisiwani Pemba Wilaya ya Mkoani.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad