HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 15, 2019

Mkazi wa Mwanza apandishwa kizimbani kwa Tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni

 
 Na Karama Kenyunko globu ya Jamii
MKAZI wa Mwanza, Emmanuel Mahumbi (38)  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka ya kuchapisha taarifa za uongo  kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Akisoma hati ya mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando.
 Wakili wa Serikali, Ester Martin amedai mshitakiwa ametenda kosa hilo katika tarehe isiyofahamika Septemba, mwaka jana jijini Dar es Salaam.

Imedaiwa, siku ya tukio mshtakiwa Mahumbi alichapisha maneno kupitia ukurasa wake wa facebook  kuwa "kichaa m1 anatoa kafara kiboya kweli 1/kaenda kumuona dada yake Bugando kumbe ndo anaenda kumkabidhi Freemason cku 2 baada ya kumuona akafa nakufa 2/kaenda kuwatembelea Ukerewe cku 2 tu baada ya kuwaona wakafa nakufa kumbe alikwenda kuwakabidhisha Freemason boya kweli liambieni libadilike litamaliza watu" huku akijua kuwa maneno hayo uongo na yana kusudi la kupotosha jamhuri.

Hata hivyo, mshitakiwa amekana kutenda makosa hayo na upande wa mashitaka umedai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo waliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Wakili wa utetezi, Hekima Mwasipu almeiomba mahakama impatie dhamana mshitakiwa kwa sababu makosa yake yanadhaminika kisheria.

Akisoma masharti ya dhamana, Hakimu Mmbando amemtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotoka ofisi zinazotambulika ambao watasaini bondi ya Sh milioni 10 na kuwasilisha hati zao za kusafiria. Haya hivyo mshtakiwa amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi imeahirishwa hadi Februari 28, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad