HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 4 February 2019

Mashindano ya kuogelea ya Taliss-IST kufanyika Februari 9 na 10

Mashindano ya kuogelea ya Taliss-IST yamepangwa kufanyika kwenye  bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga kwa siku mbili kuanzia Februari 9.

Mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji wenye umri tofauti kwa mujibu wa meneja wa klabu ya Taliss-IST, Hadija Shebe. Hadija alisema kuwa wanatarajia kupata ushindani mkubwa katika mashindano hayo ambayo yameandaliwa kwa ajili kupima maendeleo na uwezo wa waogeleaji baada ya kufanya mazoezi.

Alisema kuwa klabu yao imejipanga kuendesha mashindano yenye ushidani mkubwa chini ya usimamizi wa Chama Cha Kuogelea nchini (TSA). Alifafanua kwa wanatarajia kupata waogeleaji kutoka mikoa mbalimbali ikiwa pamoja na Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Zanzibar.

“Haya mashindano ya kupima maendeleo ya waogeaji wenye umri tofauti na maandalizi yake yamekwisha kamilika. Waogeleaji watashindana katika staili tano tofauti na vile vile kushindana kwenye ‘relay’,” alisema Hadija. Alisema kuwa kila klabu inatakiwa kuorodhesha majina ya waogeleaji wake wakiwa na umri na aina ya mashindano ambayo wanatakiwa kushindana ili kuwawezesha kuandaa programu kamili ya mashindano hayo.

Staili ambazo waogeleaji watashindania ni Backstroke, Butterfly, Freestyle, Breaststroke na Individual Medley (IM). Waogeleaji watakuwa katika makundi ya umri tofauti ikiwa pamoja na chini ya miaka nane (8), 9 na 10, 11 na 12, 13 na 14 na wenye miaka kuanzia 15 na zaidi.

Washindi kwa upande wa wanawake na wanaume watazwadiwa medali ikiwa pamoja na dhahabu, fedha na shaba wakati washindi wa kwanza, kwa makundi ya umri watazawadiwa vikombe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad