HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 4 February 2019

MAKATIBU WA WABUNGE MAJIMBONI WAPATIWA MAFUNZO

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Bunge Ndugu Jane Kajiru akifungua mafunzo  kwa makatibu wa waheshimiwa wabunge majimboni kwa ajili ya kujengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao.mafunzo hayo yametolewa  na Ofisi ya Bunge chini ya mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kushoto kwake  ni Mratibu wa Mradi wa LSP II Ndugu Mary Lasway.
 Mtaalamu kutoa Chuo cha Utumishi wa Umma , Ndugu Dorah Chenyambuga akitoa mada kuhusu utunzaji wa nyaraka, uendeshaji wa ofisi, ufuatiliaji na tathimini kwa makatibu wa waheshimiwa wabunge majimboni. Mafunzo hayo yametolewa  na Ofisi ya Bunge chini ya mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
 Baadhi ya makatibu wa waheshimiwa wabunge majimboni wakipatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo.mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma yametolewa  na Ofisi ya Bunge chini ya mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad