HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 5 February 2019

CCM PWANI YAPOKEA WANACHAMA WAPYA 250 MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 42

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) MKOA WA Pwani Kimepokea Wanachama 250 kutoka vyama vya upinzani katika maadhimisho ya sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga.

 Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo pamoja na kuwapokea wanachama hao wapya Mwenyekiti wa CCM MKOA Wa Pwani Ramadhani Maneno amewapongeza na kuwakaribisha wanachama hao wapya kuwa CCM ni chama bora nchini hivyo hawakukosea kufanya maamuzi ya kujiunga na chama hicho.

Waziri wa Tamisemi na Mbunge wa Kisarawe,Mh.Suleiman Jafo akizungumza na wananchi wa mkoa wa Pwani kuhusu changamoto zote zinazohusiana na wizara yake yeye akishirikiana na Naibu Waziri Wake Mwita Waitara watahakikisha wanatatua matatizo yote na kuwaomba watanzania wawaombee wao na Rais Magufuli Wawe na Afya njema watekeleze majukumu yao kwa asilimia 100%. 

"Ndugu zangu wanaccm wapya nawapongeza kwa kujiunga na chama dume chama tawala cha CCM na tena msijutie kujiunga na chama hiki kwa kuwa tunaye Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa na Rais wa Jamburi ya Muungano wa Tanzania,Cde Dk.John Magufuli ambaye tangu aliposhika hatamu mambo mengi mazuri ameyafanya tena yanaonekana hivyo karibuni tuijenge Pwani yetu" Alisema Mwenyekiti Maneno.

 Pia Mwenyekiti Maneno Amewataka Wanachama wote wa chama hicho kuacha tabia ya kujipitisha pitisha kutaka nafasi ya udiwani na ubunge na kuwataka mara moja kuacha tabia hiyo mara moja na kuwasisistiza muda wa wao kutembea kwa wanananchi na wanachama kujinadi bado akasema kwa mwanachama yeyote wa CCM anayejipitisha na kujinadi kutaka nafasi yeyote kati ya hizo alizozisema anafanya makosa na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake.

 Naye Naibu Waziri wa Nishati Subirá Mgalu amesema kuwa Serikali ya Dk. John Magufuli kupitia wizara yake inahakikisha inasambaza umeme nchi nzima katika mkoa wa Pwani mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme stigle gorge umezinduliwa utakapokamilika pale Rufiji utafanikisha maeneo mengi nchini kuwa na umeme wa uhakika. 

Hata Hivyo Waziri wa Tamisemi na Mbunge wa Kisarawe,Mh.Suleiman Jafo amewahakikishia wanapwani na nchi kwa ujumla kuhusu changamoto zote zinazohusiana na wizara yake yeye akishirikiana na Naibu Waziri Wake Mwita Waitara watahakikisha wanatatua matatizo yote na kuwaomba watanzania wawaombee wao na Rais Magufuli Wawe na Afya njema watekeleze majukumu yao kwa asilimia 100%. 

Akizungumza wakati akisoma risala ya wilaya ya Mkuranga Katibu wa CCM wilaya hiyo,Hakimu Jackson alisema kuwa kutokana na utaratibu wa kila wilaya,kata na matawi kuwa na vitega uchumi ili chama kiondokane na mfumo wa kuombaomba amemshukuru mbunge wa jimbo lá Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega na família yake kwa kuisaidia chama wilaya kwa kujenga vibanda vya fremu 11,ukuta na ukumbi wa kisasa ambao utaiwezesha chama kuongeza mapato yake. 

"Ndugu Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno vibanda hivi vyote,fremu 11 na uzio hivi vyote kwa pamoja vimejengwa kwa thamani ya Sh. Milioni 34,686,500 kwa fedha yake Mwenyewe mh.Mbunge Ulega bila kusaidiwa na mtu yeyote" Alisema Katibu Jackson Aidha Katibu Jackson aliongeza kwa kusema kuwa pamoja na kujenga ukuta na vibanda vya fremu pia mh.Ulega anaendelea na ujenzi wa ujenzi wa ofisi za kata 19 Kátia ya kata 25 ambapo ametumia Sh.Milioni 20,930,000 ukijumlisha fedha alizotoa kata na wilaya jumla ni Sh.Milioni 55,616,500 kitendo hiki anachokifanya mbunge ulega kinapaswa kuigwa na wabunge wengine wa CCM nchi nzima.

Kwaupande wake mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni naibu waziri wa Mifugo na uvuvi Abdalah Ulega ambaye amechangia gharama za ujenzi wa ukuta na fremu katika jengo la ccm amesema ujenzi huo utasaidia kukuinua chama hicho kiuchumi.Ulega amesema jengo hilo lililogharimu zaidi ya milion hamsini,amelijenga kwa mapenzi yake na chama cha Mapinduzi CCM.

Hata hivyo amewashukuru viongozi wote wa wilaya ya Mkuranga akiwemo Mkurungenzi wa halmashauri na diwani wa Mkuranga kwa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha ujenzi huyo.Sherehe za kumbuku za kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi kutimiza miaka 42 kwa mkoa wa Pwani,imebeba kaulimbiu isemayo kazi ni kipimo cha utu, kazi,tulinde uhuru wetu.nae,Ahmed Salum kada wa chama cha Mapinduzi amempongeza mbunge kwa jitihada kubwa anzozifanya za kuendelea ilani ya chama hicho ameahidi kumuunga mukono katika miladi mbalimbali ya unjezi wa ofisi za chama. Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Pwani,Ramadhani Maneno akiwahutubia wakazi wa Pwani na vitongoji vyake ndani ya uwanja wa (CCM) Mkuranga,wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani, ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga. Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi Mbalimbali wa Kitaifa. Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Pwani,Ramadhani Maneno akiwaongoza wakazi wa mkoa Pwani kufyeka majani eneo la Hospital ya wilaya ya Mkuranga wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga. Semu ya viongozi mbalimbai wakiwa meza kuu. Sehemu ya wananchi walio hudhuria wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga. (Picha zote na Emmanuel Massaka,MMG) Naibu Waziri wa Nishati Subirá Mgalu akizungumza na wananchi wa mkoa Pwani kuhusu mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme Stigle Gorge utakapokamilika utanufaisha maeneo mengi nchini kuwa na umeme wa uhakika. Ahmed salum kada wa chama cha Mapinduzi akimpongeza mbunge kwa jitihada kubwa anzozifanya za kuendelezaa Ilani ya chama hicho,aidha ameahidi kumuunga mkono katika miradi mbalimbali ya ujezi wa ofisi za chama. Maandamano yakiendelea sambamba na ubebaji wa mabango yenye Ujumbe wa mbalimbali.(Picha zote na Emmanuel Massaka,MMG) Sehemu ya wananchi walio hudhuria wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga. Semu ya viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad