HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 14 February 2019

Bodi inueni Stamico kwenda kibiashara zaidi-Waziri Biteko

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri wa Madini Dotto Biteko ameiagiza Bodi ya Shirika la Taifa la Madini (Stamico) kuhakikisha inafanya kazi ya kuliinua Shirika kuwa la kibiashara.
Biteko aliyasema hayo wakati akizindua Bodi ya Stamico jijini Dar es Salaam amesema Shirika limekuwa likijiendesha kwa hasara huku serikali ikifanya uwekezaji na kushindwa kutoa gawio.

Amesema Stamico ihakikishe inaongeza mchango kwenye Pato la Taifa kwa kulipia mrahaba na kodi mbalimbali za serikali pamoja na kuongeza ajira kwa watanzania kupitia uwekezaji katika sekta ya Madini. Biteko amesema kuwa wakurugenzi waliopo wana kaimu kwa muda mrefu ambapo kukaimu kwao huko kunatokana na Shirika kushindwa kuzalisha na wasipoleta matokeo wataendelea kukaimu.

Aidha ameitaka bodi kushughulikia hisa  za kampuni ya Tanzania Industries Ltd (TGI) ambapo Stamico ina umiliki lakini ilikuwa haifuatiliwi tangu ilivyosajiliwa mwaka 1969. Amesema kuwa GTI ni Kampuni Tanzu ya ilisajiliwa na Stamico mwaka 1969 kwa kujishughulisha na uchimbaji wa Madini ya Vito na ilikuwa inamiliki Kampuni ya Mundarara Ruby Mining Limited kwa ubia wa asilimia 50 kwa 50 na kampuni ya Tan Ruby na Germstone.

Biteko amesema Mundarara inamiliki kitalu cha madini ya Ruby wilayani Longido ilijiendesha kwa hasara mpaka kufikia kufilisiwa na benki ya TIB kwa uangalizi wa PCRC lakini TGI bado iko chini ya Stamico
Nae Mwenyekiti wa Bodi wa Stamico Meja Jenerali Mstaafu Michael Isanhyo amesema kuwa watahakikisha wanasimamia mikataba yote watayoingia kwa umakini. Amesema kuwa watahakikisha Shirika linatoa gawio kwa serikali kufikia Juni mwaka huu.

Isanhyo amesema Shirika hilo watakuwa wabunifu katika kuhakikisha linafanya vizuri kwa Maendeleo ya Taifa na kuonyesha imani kwa aliyemteua pamoja na wajumbe walioteuliwa.
 Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Shirika la Taifa la Madini(Stamico) kabla ya uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Stamico jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Madini Stanislaus Nyongo akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Stamico jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Menejimeti ya Stamico katika uzinduzi wa Bodi ya Stamico.


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad