HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 22, 2019

AFISA TAWALA WA WILAYA YA KISARAWE APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA RUSHWA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani imemfikisha Mahakamani John Mwendamaka, Afisa Tawala Wilaya ya Kisarawe kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kiasi cha shilingi milioni mbili (TZS 2,000,000/=) kinyume ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007.

John Mwendamaka alifunguliwa kesi ya Jinai Namba 22 ya mwaka 2019 akiwa Afisa Tawala katika ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kisarawe Devotha Kisoka, Mwendesha Mashtaka kutoka TAKUKURU, Naftali Mnzava ameieleza Mahakama kwamba mshtakiwa alitenda kosa la kuomba rushwa ya kiasi cha shilingi milioni mbili (TZS2,000,000/=) kutoka kwa mtoa taarifa ili aweze kumsaidia mdogo wake kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, jambo ambalo ni kosa kisheria kinyume na Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007.

Mnzava ameieleza Mahakama kwamba mshtakiwa alipokea rushwa ya kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mbili (TZS 2,000,000/=) kutoka kwa mtoa taarifa, jambo ambalo pia ni kosa kisheria kinyume na kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007.

Mshtakiwa amekana makosa yote mawili na dhamana ilikuwa wazi, hivyo mshatakiwa amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Kesi hii itakuja kwa ajili ya hoja za awali tarehe 05/03/2019.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani, Bi Suzana Raymond amewaasa wananchi wote kufuata taratibu kanuni na Sheria za nchi ili kuweza kwenda na kasi ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Mh Dr.John Pombe Magufuli. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad