HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 28 January 2019

WAZIRI BITEKO AANZA KUTATUA MGOGORO KATI YA MZEE MCHATA NA KAMPUNI YA MANTRAC

Waziri wa Madini, Doto Biteko leo Januari 28, amekutana na Mzee Eric Mchata na Kampuni ya madini ya Uranium ya Mantra Tanzania kwa lengo la kutatua mgogoro uliopo baina ya pande hizo mbili.

Kikao hicho, kinafuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Januari 22 na  Mzee Mchata wakati wa mkutano wa Kisekta ulioshirikisha wachimbaji wadogo na wadau wa madini uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Wakati akisikiliza kero za wachimbaji na wadau wa madini walioshiriki kikao hicho, Rais Magufuli alipokea kero ya Mzee Mchata aliyemweleza kwamba amekuwa na mgogoro na kampuni hiyo kwa kipindi cha takribani miaka 12 na bado hajapata suluhu. Akijbu kero iliyowasilishwa na Mzee Mchata, Rais Magufuli aliitaka Wizara ya Madini kuhakikisha mgogoro huo unafikia mwisho.
 Waziri wa Madini Doto Biteko akimweleza jambo Mzee Eric Mchata wakati wa kikao cha kusuluhisha mgogoro baina yake na kampuni ya Mantra Tanzania.
Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mzee Eric Mchata. Kulia aliyekaa ni Meneja Maendeleo, Utawala na RasilimaliWatu wa kampuni ya Mantra Tanzania, Phillemon Tano.
 Sehemu ya Wataalam wa wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini wakifuatilia kikao cha kusuluhisha mgogoro kati ya kampuni ya Mantra na Mzee Eric Mchata. Kutoka kulia ni Kamishna wa Tume ya Madini, Prof. Abdulkarim Mruma, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na Afisa Sheria wa Wizara ya Madini, Joseph Nyamsenda. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad