HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 12 January 2019

WANAFUNZI WA KIKE 235 MKOANI PWANI WAPATA MIMBA KIPINDI CHA MWAKA 2018

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
WANAFUNZI wa kike 235 wa shule za msingi na sekondari mkoani Pwani wamepata mimba katika kipindi cha mwaka 2018 ,hali ambayo ni mbaya. Kutokana na takwimu hiyo, kamati ya ushauri ya mkoa wa Pwani (RCC) imekemea vikali masuala ya mimba za utotoni ,na kuagiza sheria ichukue mkondo wake kwa wale ambao wamehusika kuwapa mimba wanafunzi hao.

Akizungumza kwenye kikao cha ushauri cha mkoa huo, ofisa elimu mkoa wa Pwani, Abdul Maulid alisema kati ya wanafunzi hao, 155 ni wanafunzi wa shule za sekondari. Alieleza, wanafunzi wengine 80 waliopata mimba katika kipindi hicho ni wa shule za msingi. "Mikoa ya wenzetu kama Kilimanjaro tujiulize kwanini wanafunzi hawapati mimba ,tushirikiane kupiga Vita tatizo hili ,"

"Madereva bodaboda, jamii ishirikiane na serikali kupambana na namba hii, bodaboda msiwe chanzo cha kupakia wanafunzi hawa na kuwarubuni kuwapa mimba "alisisitiza Maulid. Hata hivyo, alielezea, changamoto ya shule kuwa umbali mrefu, wanafunzi kukosa chakula mashuleni ni chanzo moja wapo cha wanafunzi kupata mimba. 

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema vyombo vya dola visiwafumbie macho wahusika wa mimba hizo. Alisema, namba hiyo ni kubwa hivyo sheria ichukue mkondo wake na wafungwe miaka 30 jela ili iwe fundisho. Ndikilo anawataka ,wazazi na walezi kuacha kumalizana kesi za mimba za utotoni majumbani na kurubuniwa fedha ili kuwaachia huru wanaobainika kuwapa mimba watoto wao wakike. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad