HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 27 January 2019

UJUMBE WA MFUKO WA SHEIKH KHALIFA FUND FOR ENTERPRISE DEVELOPMENT WATEMBELEA ZANZIBAR

MKURUGENZI wa Mfuko wa ‘KhalifaFund’ Naizar Cheniour, amesema mfuko huo umeazimia  kuwawezesha vijana wa Zanzibar katika nyanja mbali mbali za kiuchumi ili kuweza kujiajiri na kuinua hali zao za maisha.

Mkurugenzi huyo amesema hayo leo wakati  alipozungumza na waandishi wa habari, mara baada ya ujumbe wa Mfuko huo ulipowasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Ujumbe huo upo nchini kwa ziara maalum, ikiwa ni muendelezo wa mazungumzo na Serikali, yenye lengo la kufanikisha utekelezaji wa programu mbali mbali katika sekta za biashara, ujasiriamali, miundombinu na nyenginezo.

Alisema Mfuko umelenga kuwawezesha vijana wa Zanzibar katika upatikanaji wa rasilimali fedha, utaalamu na masuala ya kiufundi ili waweze kujiajiri kupitia shughuli za ujasiriamali na hivyo kuweza kujitegemea.

Aliwataka vijana na Wazanzibari kwa ujumla kutarajia mafinikio makubwa kutokana na  program mbali mbali zitakazotekelezwa kupitia Mfuko huo.

Alisema mfuko wa KhalifaFund, una uzoefu mkubwa katika utekelezaji wa programu za maendeleo na shughuli za kiuchumi, ambapo umekuwa ukifanya kazi hizo katika nchi mbali mbakli duniani.

Mapema, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda, Dk. Juma Ali Juma alisema ujio wa Viongozi wa Mfuko wa’ KhalifaFund’  umelenga kukamilisha mazungumzo yaliofikiwa katika kikao kilichopita ili kuwa tayari kwa utekelezaji wa yale yalioafikiwa.

Alisema mfuko huo wa kifedha, wenye makao makuu yake Abu Dhabi ,UAE utatowa msukumo mkubwa  katika utekelezaji wa program mbali mbali za kimaendeleo na kiuchumi, sambamba na kuwawazesha vijana kupitia kazi za ujasiriamali.

Alisema wakati ukiwa nchini utakutana na kufanya mazungumzo na taasisi mbali mbali za Serikali pamoja na kutembelea maeneo tofauti.

Hii ni mara ya pili kwa viongozi wa Mfuko wa ‘KhalifaFund’ kuja nchini kwa ajili hiyo, ambapo kabla ulipata fursa ya kutembelea sekta tofauti za maendeleo na kiuchumi Unguja na Pemba.

Aidha, ujio wa mfuko huo unafutia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein aliyoifanya Umoja wa nchi za Falme ya Kiarabu (UAE) Januari mwaka uliopita. 
 

 KATIBU Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg.Juma  Ali Juma, akisalimiana na Afisa wa Mfuko wa Khalifa Fund for Enterprise Development Ndg. Abdulah Al Jarwani, wakati wakiwa sili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kwa ziara ya siku tatu kutembelea Miradi mbalimbali Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 KATIBU Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg Juma Ali Juma, akizungumza na Ujumbe wa Mfuko wa Khalifa Fund for Enterprise Development ya Abudha Dhabi UAE, ulipowasili Zanzibar kwa ziara ya Siku Tatu ukiongozwa na Mkurugenzi Nizar Cheniour, mwenye fula nyeusi. wakiwa katika ukumbi wa VIP uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, baada ya kuwasili kwa ziara ya siku tatu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 KIONGOZI wa Mfuko wa Khalifa Fund for Enterprise Development wa Abu Dhabi UAE, ukiongozwa na Mkurugenzi Ndg. Nazar Cheniour, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, kutembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 AFISA wa Mfuko wa Khalifa Fund for Enterprise Development Ndg. Ali Al Saad, akipata maelezo ya kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushirika wa Fakirice Milling Enterprises wa Kisongoni Ndg. Yussuf Faki Yussuf, akitowa maelezo ya usagaji wa mpuga katika ushirika wao wakati walipotembelea ushirika huo leo.(Picha na Ikulu)
KATIBU Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Ndg Juma Ali Juma, akitowa maelezo kwa Kiongozi wa Ujumbe wa Mfuko wa Khalifa Fund for Enterprise Development Ndg. Nizar Cheniour, walipotembelea Ushirika wa Fakirice Milling Enterprises Kisongoni,unaojishughulisha na kukoboa mpunga.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad