HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 11, 2019

Tazama Coppa Italia kwenye StarTimes pekee

Ronaldo kuanza kazi dhidi ya Bologna Katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Coppa Italia ni timu mbili tu zinatoka Serie C huku zikikutana na vilabu kutoka jijini Roma, Novara watakaocheza dhidi ya Lazio huku Virtus Entella wakicheza dhidi ya AS Roma siku ya Jumatatu.

Timu nyingine ambayo haitokei Serie A ni Benevento ambao watasafiri kuelekea Milan ambako watacheza dhidi ya Inter. Huku ikitarajiwa kwamba vilabu vingi vikubwa vitashinda, mechi kati ya Bologna na Juventus itakuwa kivutio zaidi. Juventus tayari wako kileleni mwa Serie A wakiwa alama 9 mbele ya Napoli ambao wako nafasi ya pili.

Klabu hiyo ya jijini Turin itataka kujihakikishia ushindi dhidi ya Bologna ambao ni wa tatu kutoka mwoisho katika msimamo wa Serie A, ili wawe katika nafasi nzuri ya kushinda kombe hilo kwa mara ya 14.

Kikosi cha Massimilano Allegri bado hakijapoteza mchezo wowote katika ligi za ndani kwa msimu huu, huku kikosi chao kikiwa na utajiri hasa eneo la ushambuliaji wachezaji kama Cristiano Ronaldo, Paulo Dybala na Mario Mandzukic, itakuwa jambo la kushangaza endapo watapoteza mchezo huo licha ya kuwa ugenini.

Ronaldo amefunga jumla ya magoli 14 katika ligi, goli moja pungufu ya magoli ambayo kikosi kizima cha Bologna kimefunga (15), mreno huyo amekuwa katika kiwango kizuri tangu alipowakacha mabingwa wa Ulaya Real Madrid. Mchezo mwingine wenye burudani utapigwa jijini Genoa ambapo Sampdoria watacheza dhidi ya AC Milan siku ya Ijumaa.

Wapenzi wa Soka nchini wataweza kutazama mechi hizi kupitia StarTimes pekee. Mechi kati ya Bologna na Juventus itachezwa Jumapili saa 2 Usiku na kurushwa moja kwa moja kupitia ST World Football pekee, ambapo wateja watatakiwa kulipia kifurushi cha MAMBO Tsh 14,000 kwa watumiaji wa Antenna na SMART Tsh 21,000 kwa watumiaji wa Dish.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad