HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 25 January 2019

TANESCO YAPONGEZWA KWA KUIMARISHA HUDUMA ZAKE ARUSHA

Mkurugenzi kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Bw. Sailesh Pandit
Meneja Uendeshaji wa kiwanda cha Sunflag Bw. Magessa Charles(kulia), akifafanua jambo kuhusu utengenezaji wa nguo
Wafanyakazi wa kiwanda cha A -Z wakiwa kazini
Meneja Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, anayeshughulikia miradi, Mhandisi Emmanuel G. Munirabona(kulia), akizungumza na Mkurugenzi kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Bw. Sailesh Pandit.Picha zote nz Vero Ignatus

Na.Vero Ignatus Arusha
Shirika la umeme nchini Tanzania TANESCO limepongezwa kwa kuimarisha huduma zake kwa wateja wa wakubwa na wale wa kati jijini Arusha 
Akizungumza Mkurugenzi kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Bw. Sailesh Pandit amesema huduma za TANESCO zimeimarika kiasi kwamba ameshawishika kufungua viwanda vingine vitatu Jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga

“Zamani tulikuwa na shida sana miaka miwili mitatu iliyopita, power cut (kukatika kwa umeme), sasa hivi hamna ni mara chache sasa labda ikitokea kwenye gridi ya taifa hapo hatuna ha kufanya, lakini sasa hivi hatuna tatizo la umeme kabisa.” Alisema Bw. Sailesh ambaye kwa mwezi anailipa TANESCO kiasi cha kati ya shilingi milioni 500 hadi 600 kama bili ya umeme.

Akizungumzia ushirikiano wa kikazi kutoka kwa wafanyakazi wa TANESCO na kiwanda chake, Bw. Sailesh amesema, hakuwahi kuuona ushirikiano huo miaka ya nyuma ila ndio ameanza kuona hivi sasa ambapo inawatia moyo wao kama wawekezaji na kuona wanaifikia Tanzania ya viwanda

“Kwakweli sina cha kusema au kibaya chochote, namna ninavyofanya kazi nao ni very friend manner, mimi ninaweza kumpigia simu Injinia hata saa nane usiku, sina umeme ata respond simu yako hapo hapo na kuchukua hatua wakati kipindi cha nyuma haikuwa hiovyo.” 

Hali kadhalika uongozi wa kiwanda cha nguo Sunflag, nao umetoa pongezi kwa TANESCO kwa kusema kuwa huduma zimeboreka na kwamba kuna matatizo madogomadogo tu.

“Nina kila sababu ya kuwashukuru TANESCO kipindi cha nyuma kila mtu ni shahidi tulikuwa na matatizo kwenye eneo hili la upatikanaji wa umeme lakini pia ushirikiano haukuwa mzuri sana, lakini kwa sasa, panapotokea tatizo response ya TANESCO panapotokea tatizo ni ni very fast na very incouraging mtu atakayewanyooshea kidole itakuwa ni sababu zake mwenyewe.”

Alipongeza pia mfumo wa utoaji taarifa, ambapo hata kama kuna katizo la umeme wamekuwa wakipata taarifa mapema na wao kama kiwanda hujipanga na hivyo kuondoa usumbufu.

Aidha uongozi wa kiwanda cha A to Z pamoja na kuponegza kuimarika kwa upatikanaji wa umeme, wao bado kuna wakati umeme unapungua nguvu (fluctuation) na hivyo kusababisha mitambo yao kusimama kufanya kazi

“Lakini kwa ujumla kumekuwa na maendeleo mazuri ya hali ya umeme ukilinganisha na kipindi cha nyuma, wito wetu ni kufanyia kazi mapungufu hayo,” Alisema Afisa Mterndaji Mkuu wa A to Z, Bw.Viral Shah.

Akizungumzia mapungufu hayo, Meneja Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, anayeshughulikia miradi, Mhandisi Emmanuel G. Munirabona, alisema wao kama shirika watafuatilia kwa kina kujua hasa nini chanzo cha tatizo hilo.

“Tumefanya maboresho makubwa ya mitambo yetu ikiwa ni pamoja na kupanua vituo sita vya kupoza umeme jijini Arusha, ambavyo vimewezesha wateja wakubwa kufunguwa laini zinazojitegemea ili kuondoa uwezekano wa kukatika kwa umeme na hivyo kuathiri shughuli za uendeshaji

Jiji la Arusha ni miongoni mwa miji mitatu ambayo ilikuwa kwenye mpango wa kukarabati na kuimarisha miundombinuya umeme (TEDAP), ambapo Shirika hilo lilifanya ukarabati mkubwa wa njia za kusafirisha umeme lakini pia kufanya upanuzi wa vituo vya kupoza umeme.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad