HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 30, 2019

Sheria ya Ardhi ya Kilimo Itapunguza Migogoro ya Wakulima

Na Bashiri Salum, Dodoma
Sehemu kubwa ya ardhi inayotumika kwa shughuli za kilimo nchini haitambuliki kama ni ardhi ya kilimo kisheria hivyo kuwa ni chanzo cha migogoro hasa vijijini. 

Akiongea wakati wa kikao kazi cha maandalizi ya sheria ya kuanisha kulinda na kusimamia matumizi ya ardhi ya kilimo kilichofanyika katika ukumbi wa  chuo cha wakulima Bihawana hivi karibuni, Mkurungenzi wa Idara ya Usimamiaji na Mipango ya Ardhi Bwana Paulo Tarimo amesema sehemu ya ardhi inayotumiwa kwa shughuli za kilimo imekuwa ikipangiwa matumizi mengine hivyo kuwa chanzo cha migogoro hapa nchini.

Aidha tafiti za kisayansi zinaonesha kwamba zipo ikolojia mbalimbali za kilimo hapa nchini lakini  ardhi inayofaa kwa kilimo imekuwa ikipangiwa matumizi mbalimbali bila kujali mahitaji ya ardhi ya kilimo kwa matumizi ya sasa na ya baadaye alisistiza Bwana Tarimo.  Hata hivyo amesisitiza kwamba idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kwa kasi lakini ardhi haiongezeki, hivyo jitihada za dhati zinatakiwa kuchukuliwa ili  kuanisha kulinda na kusimamia ardhi hiyo kwa manufaa mapana ya kuimarisha uzalishaji na uwekezaji katika kilimo.

Aidha  amebainisha kwamba Wizara ya Kilimo kupitia Idara ya  Mipango na Matumizi ya Aridhi ya Kilimo  imekutana mara kadhaa kuandaa rasimu ya sheria ya kuainisha, kulinda na kusimamia matumizi ya ardhi ya kilimo ili kupunguza migogoro ya aridhi ambayo imekuwa ikisababishwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa matumizi mengine yasikuwa ya kilimo katika ardhi hiyo. 'migogoro mingi ya ardhi ipo vijijini ambayo inasababishwa na muingiliano wa matumizi ya ardhi ya kilimo na matumizi mengine yasiyokuwa na kilimo hivyo sheria hiyo itasaidia ardhi ya kilimo  kutambuliwa kuwa ni maalum kwa  shughuli za kilimo."

Hata hivyo ameendelea kueleza  kwamba sheria hii itakuwa na manufaa kwa wakulima na wawekezaji kwa sababu italinda  rutuba ya udongo na kuleta uendelevu wa matumizi ya ardhi hiyo kwa kuwa watumiaji watalazimika kuitumia ardhi  kwa misingi ya kanuni za kilimo bora zitakazokuwa zimeainishwa

''Sehemu kubwa ya ardhi inayotumika kwa shughuli za kilimo haitumiki kwa kupewa matunzo ya kutosha ili kuiwezesha kutumika kwa muda mrefu bila ya kuathiri rutuba na ubora wake''. aliendelea kueleza Bwana Tarimo
sheria hii ni muhimu kwa kuwa itasaidia   kuwekwa katika madaraja yatakayoainisha idadi na uwezo wa kimtaji na kiteknolojia wa wakulima wadogo, wa kati na wakubwa. Hii itaongeza tija na ufanisi katika kusimamia na kuratibu uendelezaji wa rasilimali ardhi ya kilimo nchini. 
hata hivyo uaandaaji wa rasimu ya muswada huo ulitokana na  marekebisho ambayo yalitolewa awali na kikao cha baraza la mawaziri kilicho fanyika hivi karibuni
Aidha kikao hicho kilijumuisha wadau mbalimbali ambapo matokeo ya kikao kazi hicho yatajadiliwa katika ngazi mbambali kabla ya kupelekwa katika baraza la mawaziri
Kikosi kazi  kinachoshughulikia rasimu ya muswada wa sheria ya ardhi ya Kilimo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha kazi hiyo iliyokuwa inafanyika katika ukumbi wa chuo cha wakulima Bihawana hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad