HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 31, 2019

SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KILITEX-ARUSHA

Na Saidina Msangi, WFM, Dodoma

Serikali iliwalipa stahili zote Watumishi wa Kiwanda cha nguo cha KILITEX kilichopo mkoani Arusha baada ya kufungwa kutokana na tatizo la ukosefu wa mtaji na malimbikizo ya madeni.

Hayo yamebainishwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, alipokua akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalaum Mhe. Catherine Magige, aliyeuliza ni lini Serikali itawalipa wafanyakazi 545 wa KILITEX ambao bado wanadai pensheni baada ya kiwanda hicho kufungwa ilihali mwajiri wao hakuwasilisha michango yao kwenye Mfuko wa Kijamii wa PPF.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, kwa mujibu wa kumbukumbu na nyaraka za ufilisi, taratibu za ufilisi zilikamilika na wafanyakazi hao walilipwa stahiki zao kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni  namba 46 ya mwaka 1931. 

“Baadhi ya wafanyakazi walilipwa mafao ya kiinua mgongo kwa mkupuo na wengine walirejeshewa michango yao kwa kadiri walivyochangia baada ya Mfilisi kushindwa kulipa riba, adhabu na malimbikizo ya michango kwenye mfuko wa Pensheni wa PPF”, alisema Dkt. Kijaji.

Alisema Kiwanda hicho kilisimamisha shughuli za uzalishaji mwaka 1994 na kuwekwa chini ya ufilisi na PSRC mwaka 1995.

Aidha akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlimba, Mhe. Suzan Kiwanga, alietaka kufahamu ni lini wafanyakazi 11075 wa Shirila la Reli la Tanzania na Zambia- TAZARA waliostaafishwa kwa lazima miaka 55 mwaka 2005, watalipwa mafao yao.

Alisema Serikali imefuatilia madai hayo na takwimu sahihi ni wastaafu 271 walistaafishwa na madai yao yanashughulikiwa ili waweze kulipwa mafao yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad